YULE MWANAMKE WA KWANZA KUSHIKA URAIS HUKO BRAZIL ASHINDA TENA

Dilma 
Mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa urais nchini Brazil 2011, Diana Rousseff amechaguliwa tena kushika wadhifa huo katika uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumapili Oktoba mwaka huu nchini humo.

Baada ya kutangazwa kushinda katika kinyang’anyiro hicho, Rousseff mwenye umri wa miaka 66 amesema anahitaji kufanya vizuri katika awamu hii ya uongozi wake huku akisifia jitihada zake na rais aliyemtangulia Luiz Inacaio Da Silva kuwa katika vipindi vyao vya uongozi wametatua tatizo la ajira kwa kiasi kikubwa.

Rousseff ameshinda kwa 51.59% ambapo mpinzani wake Aecio Neves amepata kura 48.41%.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post