Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALI PICHA- MAADHIMISHO YA SIKU YA MLIPA KODI MKOA WA SHINYANGA LEO

Hapa ni katika viwanja vya Shy-Com mjini Shinyanga ambako leo kumefanyika maadhimisho ya nane ya siku ya walipa kodi mkoa wa Shinyanga yaliyohudhuriwa na wafanyabiashara mbalimbali kutoka mkoa huo huku wadau wa mamlaka ya mapato nchini nao wakihudhuria ambapo mgeni rasmi alikuwa kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annarose Nyamubi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga-picha na Kadama Malunde
Awali kaimu meneja mamlaka ya mapato(TRA) mkoa wa Shinyanga Norbertus Tizibazomo akimkaribisha mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku Mlipa kodi yaliyoanza rasmi tarehe 17,Novemba 2014 yakiwa na kauli mbiu "Risti ni Haki yako asiyetoa anakwepa kodi".Maudhui yake yakiwa ni kuhamasisha utoaji risti sahihi kwa mauzo ya bidhaa na huduma mbalimbali na pia kumkumrusha kila anayefanya malipo ya bidhaa na huduma kudai risti kwa kila manunuzi anayofanya-picha na Kadama Malunde

Wafanyabishara,wafanyakazi wa TRA mkoa wa Shinyanga na wadau wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika viwanja vya Shycom leo-picha na Kadama Malunde
 
Mgeni rasmi Annarose Nyamubi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizungumza wakati wa maadhimisho hayo.Pamoja na mambo mengine aliwataka wafanyakazi wa TRA kufanya kazi kwa uadilifu wakifuata sheria na kanuni zilizopo-picha na Kadama Malunde
Nyamubi pia aliwataka wafanyabishara kutoa risti sahihi kwa mauzo na manunuzi sahihi huku akiwaasa wananchi kujenga tabia ya kudai risti kila wanaponunua bidhaa kwa wafanyabiashara-picha na Kadama Malunde

Baadhi ya wageni katika jukwaa kuu leo wakifuatilia kilichokuwa kinajiri uwanjani-picha na Kadama Malunde

Burudani nayo ilikuwepo_Serengeti Band ya Shinyanga wakifanya yao-picha na Kadama Malunde

Tunafuatilia kinachoendelea-picha na Kadama Malunde

Kulia ni Mwenyekiti wa Chemba ya biashara(TCCA) mkoa wa Shinyanga Dickson Mussula akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mlipa kodi leo ambapo alisema miongoni mwa chagamoto wanazokabiliana nazo ni manispaa ya Shinyanga kutotoa elimu ya ulipaji kodi kwa wananchi na kwamba kituo cha mabasi cha Shinyanga hakiridhishi sambamba na baadhi ya ofisi za kata kuwa vituo vya kutolea rushwa akitolea mfano ofisi ya kata ya Chamaguha-picha na Kadama Malunde
Kushoto ni Kaimu meneja wa mamlaka ya mapato (TRA) mkoa wa Shinyanga Norbertus Tizibazomo akisoma hotuba.Alisema mamlaka ya mapato kwa niaba ya serikali imejizatiti katika kuongeza na kuboresha huduma zake kwa walipa kodi.Tizibazomo alisema makusanyo ya kodi yameendelea kukua mwaka hadi mwaka mfano katika mwaka wa fedha uliomalizika June 2014 walikusanya shilingi 16,979.3 milioni ikilinganishwa na shilingi 13,410.5 milioni zilizokusanywa mwaka mmoja nyuma yake-picha na Kadama Malunde
Afisa elimu wa kodi kutoka mamlaka ya mapato mkoa wa Shinyanga Anthony Faustine akitoa elimu kwa wafanyabiashara waliohudhuria maadhimisho hayo juu ya mashine za kutolea risti za EFD ambapo alisema mashine inapoharibika taarifa za kwanza kabisa zinapaswa kupelekwa wa wakala aliyeuza mashine-picha na Kadama Malunde
BAADA YA HOTUBA-Meza kuu wakiongozwa na mgeni rasmi wakijiandaa kutoa zawadi kwa wafanyabiashara/walipa kodi na taasisi na idara ambazo zilisaidia mamlaka ya mapato katika kufanikisha shughuli zake za kukusanya mapato ya serikali kwa mwaka wa fedha 2013/2014-picha na Kadama Malunde
Mgeni rasmi Annarose Nyamubi aligawa vyeti kwa baadhi ya walipa kodi waliowakilisha wenzao kwa kuonesha uadilifu wa kuridhisha katika kulipa kodi kwa mwaka 2013/2014 na hivyo kuchangia katika juhudi za taifa la Tanzania kupambana na umaskini-Pichani ni Mwakilishi wa Soud Industries limited ambao ni washindi kwa kwanza kimkoa kwa walipa kodi wakubwa-picha na Kadama Malunde

Cheti-Walichokabidhiwa Soud Industries limited ambao ni washindi kwa kwanza kimkoa kwa walipa kodi wakubwa-picha na Kadama Malunde
Mwakilishi wa Fresho Investment,washindi wa Tatu ngazi ya walipa kodi wakubwa mkoa wa Shinyanga akipokea cheti-picha na Kadama Malunde 
Mkurugenzi wa kampuni ya Ulinzi ya Zenith Security Services limited  Elisha Ndulu ambao ni washindi wa kwanza kwa walipa kodi ngazi ya kati mkoa wa Shinyanga  akipokea Cheti cha ushindi baada ya kuonesha mfano wa kuigwa kwa makampuni mengine ya ulinzi-picha na Kadama Malunde

 Zenith Security Services Limited -picha na Kadama Malunde
Mkurugenzi wa kampuni ya Ulinzi ya Zenith Security Services limited  Elisha Ndulu ambao ni washindi wa kwanza kwa walipa kodi ngazi ya kati mkoa wa Shinyanga  akionesha cheti cha Ushindi -picha na Kadama Malunde
 Bwana Ali Hamad Hilal akijiandaa kupokea cheti kwa kuwa washindi wa pili ngazi ya kati,yeye anajihusisha na biashara ya mafuta mkoani Shinyanga-picha na Kadama Malunde

Katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga ndugu Boniface Chambi akipokea cheti kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya uhamasishaji kodi mkoani Shinyanga kwa kuwa wadau wakubwa wa TRA-picha na Kadama Malunde

Mweka hazina klabu wa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Stella Ibengwe ambaye ni mwandishi wa habari gazeti la Mwananchi akitoka kupokea cheti kwa niaba ya uongozi wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga(SPC) ikiwa ni miongoni mwa taasisi zilizosaidia mamlaka ya mapato katika kufanikisha shughuli zake za kukusanya mapato ya serikali kwa mwaka wa fedha 2013/2014-picha na Kadama Malunde
 
Cheti kwa ajili ya klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga-SPC-picha na Kadama Malunde
Mwandishi wa habari na mtangazaji kutoka Radio Faraja ya Shinyanga akipokea cheti kwa niaba ya uongozi wa Radio Faraja ikiwa ni miongozi mwa taasisi zilizosaidia mamlaka ya mapato katika kufanikisha shughuli zake za kukusanya mapato ya serikali kwa mwaka wa fedha 2013/2014-picha na Kadama Malunde

ZAWADI KWA WANAFUNZI-Mwanafunzi kutoka shule ya sekondari Uhuru ambao ni washindi wa kwanza katika mashindano ya kujibu maswali(Quiz) kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kodi zinazosimamiwa na TRA, yaliyoandaliwa na mamlaka ya mapato mkoa wa Shinyanga,yakishindanisha shule 7 za sekondari tofauti katika manispaa ya Shinyanga.Washindi wa pili ni Kom sekondari,wa tatu ni Town sekondari-picha na Kadama Malunde 
Pichani ni Pius  Mhango kutoka shule ya sekondari KOM.Huyu ndiyo mshindi wa kwanza kwa wanafunzi wote walioshiriki katika mashindano yaliyoandaliwa na TRA yakiwa na lengo la kuwaandaa wanafunzi wa leo kuwa walipa kodi na watoza kodi wa siku zijazo-picha na Kadama Malunde

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com