Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA- MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA MZAZI WA MGEJA MJINI KAHAMA

<<BONYEZA MANENO HAYA TUKUTUMIE PICHA ZA VITUKO NA VICHEKESHO>>

 Msafara kuelekea kwenye msikiti mkuu wa Ijumaa mjini Kahama kwa ajili ya mwili wa marehemu kuswaliwa mchana wa leo ambapo mami ya watu kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga wamejitokeza kumzika(Bibi Halima Nchimika amezaliwa mwaka 1940) mama mzazi wa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja.Mazishi yamefanyika katika makaburi ya Uhindini mjini Kahama.Wakati mwili wa marehemu ukitolewa nyumbani mvua ilianza kunyesha muda mfupi ikakatika kabla ya kufikishwa msikitini,baada ya hapo msafara ulielekea makaburini,mazishi yakaendelea,lakini wakati yakielekea mwisho mvua ikanyesha na kusindikiza msafara hadi nyumbani kisha ikakatika-Picha na Kadama Malunde
 Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa  akisalimiana na bi Halima Nchimika enzi za uhai wake mjini Kahama nyumbani kwa Mgeja-Picha kutoka Maktaba ya Malunde1 blog
Mheshimiwa Lowassa akiwa na mama mzazi wa Mgeja(Halima Nchimika) enzi za uhai wake-picha kutoka maktaba ya Malunde1 blog

Mwili wa marehemu ukiwasili katika makaburi ya Uhindini mjini Kahama leo mchana,ambapo watu mbalimbali wenye mapenzi mema wakiwemo viongozi wa serikali,vyama vya siasa,dini na wengine wengi wamejitokeza kumzika bi Halima Nchimika(74) aliyefariki dunia jana wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza baada ya kuugua muda mrefu-Picha na Kadama Malunde

Mazishi yanaendelea-Pia mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga alikuwepo(mwenye suti nyeusi na miwani kushoto),kulia kwake ni katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga-Picha na Kadama Malunde

Mazishi yanaendelea-Picha na Kadama Malunde

Mtoto wa marehemu ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akiweka udongo kaburini kumzika mama yake Halima Nchimika aliyefariki dunia jana jijini Mwanza-Picha na Kadama Malunde

Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akiweka udongo kaburini,nyuma yake ni Boniface Butondo mjumbe wa NEC taifa,akifuatiwa na mbunge wa Kahama mjini James Lembeli-Picha na Kadama Malunde

 Mbunge wa Kahama mjini James Lembeli akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi leo mchana-Picha na Kadama Malunde
WAKATI MAZISHI YANAENDELEA MVUA IKANYESHA-,Pichani ni msafara wa waombolezaji wakitoka makaburini kuelekea nyumbani kwa Mgeja mtaa wa Nyasubi mjini Kahama huku mvua ikinyesha,ambapo wataalam wa mambo walisema hiyo ni ishara ya marehemu kupokelewa na mungu -Picha na Kadama Malunde

Nyumbani kwa mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga palipo na msiba,waombolezaji wakiwa wamekaa baada ya mazishi kusubiri utaratibu mwingine-Picha na Kadama Malunde
Kushoto ni kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha akiwa msibani leo-picha na Kadama Malunde
 Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja katika mtaa wa Nyasubi mjini Kahama-Picha na Kadama Malunde
Sheikh wa mkoa wa Shinyanga Ismail Habibu Makusanya akizungumza baada ya mazishi-Picha na Kadama Malunde

Mbunge wa Msalala wilayani Kahama Ezekiel Maige ambaye ni mwenyekiti wa wabunge wanane wa mkoa wa Shinyanga akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya wabunge wenzake-Picha na Kadama Malunde

 Mbunge wa Msalala wilayani Kahama Ezekiel Maige akiteta jambo na mbunge wa Kahama mjini James Lembeli -Picha na Kadama Malunde
Mbunge wa Kahama mjini James Lembeli akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya wananchi wa Kahama-Picha na Kadama Malunde

Mbunge wa Kahama mjini James Lembeli(kushoto) akiwa amekumbatiana na mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga baada ya kutoa salamu za rambirambi na kumpa pole kwa kufiwa na mama yake mzazi-Picha na Kadama Malunde

Mbunge wa Kishapu Suleiman Masoud Nchambi akizungumza baada ya mazishi nyumbani kwa Mgeja leo-Picha na Kadama Malunde

Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa Mgeja leo-Picha na Kadama Malunde

 Aliyeshikilia kipaza sauti(wa nne kutoka kushoto) ni Mjumbe wa halmashauri kuu CCM taifa  Dkt Rafael Masunga Chegeni akiwa na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM kutoka kanda ya ziwa nyumbani kwa Mgeja leo-Picha na Kadama Malunde
Mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele ambaye pia ni naibu waziri wa madini nchini akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya serikali ya muungano wa Tanzania leo-Picha na Kadama Malunde

Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa Mgeja leo-Picha na Kadama Malunde

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindayi ambaye ni mwenyekiti wa wenyeviti nchini akizungumza kwa niaba ya wenyeviti wenzake.pia alitoa salamu za rambi rambi kutoka kwa mheshimiwa Edward Lowassa waziri mkuu mstaafu,ambaye ni mbunge wa Monduli -Picha na Kadama Malunde

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindayi ambaye ni mwenyekiti wa wenyeviti akimpa mkono wa pole mtoto wa marehemu( Khamis Mgeja )leo-Picha na Kadama Malunde
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akito neno la shukrani kwa watu wote walioshiriki katika msiba huo-Picha na Kadama Malunde

Waombolezaji wakiwa msibani leo-Picha na Kadama Malunde

Waombolezaji wakiwemo viongozi wa dini wakiwa nyumbani kwa Mgeja leo-Picha na Kadama Malunde

Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa Mgeja leo-Picha na Kadama Malunde

Mjumbe wa halmashauri kuu CCM mkoa wa Richard Masele Msanii(mwenye kofia kushoto) aliyemwakilisha mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum akiwa na mkuu wa wilaya ya Kahama ndugu Benson Mpesya,nyuma yao ni meneja wa Kahama Fm ndugu Marco Mipawa-Picha na Kadama Malunde

Baada ya mazishi -Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika picha ya pamoja na mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga,wa kwanza kulia ni mkurugenzi wa Malunde1 blog,ndugu Kadama Malunde-Picha na Mohab Dominic

Waandishi wa habari nao walikuwepo,wa kwanza kushoto ni Mohab Dominic gazeti la Nipashe,katikati ni Chibura Makorongo mwandishi wa habari gazeti la Uhuru na Mzalendo,akifuatiwa na Kadama Malunde mwandishi wa gazeti la Mtanzania pia mkurugenzi wa Malunde1 blog.Waandishi wengine hawako pichani ambao ni Raymond Mihayo gazeti la Habarileo na Ali Lityawi gazeti la Tanzania Daima na Ndalike Sonda kutoka Radio Kahama-Picha na Ndalike Sonda

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com