Mazishi ya mwanafunzi Yunis Festo aliyekuwa anasoma kidato cha nne katika shule ya sekondari Simba wa Yuda iliyoko katika kijiji cha Bulima wilaya ya Busega yamefanyika mchana huu katika kijiji cha Igembe wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza .
Watu mbalimbali wenye mapenzi mema wakiwemo walimu,wanafunzi,viongozi wa dini na wakazi wa kijiji hicho na wengine kutoka mikoa ya jirani wamehudhuria mazishi hayo.
Ibada ya mazishi imeongozwa na mchungaji Josephares Ihoneyo Mtebe.
Yunis Festo aliyezaliwa tarehe 26.02.1996 amefariki dunia juzi saa 11 alfajiri zikiwa zimesalia saa tatukuanza kufanyika kwa mtihani wa kidato cha nne kote nchini ulioanza juzi Jumatatu.
Malunde1 blog iliiambiwa kuwa mwanafunzi huyo amefariki dunia juzi baada ya kukimbizwa katika kituo cha afya Bulima na wanafunzi wenzake aliokuwa nao bwenini alipozidiwa majira ya saa 9 usiku wa kuamkia siku ya Jumatatu.
Habari zinasema kuwa mwanafunzi huyo alikuwa anaumwa kichwa na kwamba alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Sickle Cell.
Malunde1 blog inawapa pole ndugu,jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huo.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Yunis Festo.Amina
PICHA/HABARI NA DAMIANI KAGEBA LUPIMO
Malunde1 blog inawapa pole ndugu,jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huo.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Yunis Festo.Amina
PICHA/HABARI NA DAMIANI KAGEBA LUPIMO
Social Plugin