BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU TUNAPOZIWEKA
Hapa ni katika ukumbi wa Ibanza Hotel mjini Shinyanga ambako leo kumefanyika mkutano mkuu wa mwaka wa Shirika la Agape Aids Control Programme(AACP),ambalo ni shirika lisilo la kiserikali,kisiasa wala kidini linalojihusisha na kuratibu masuala ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na madhara ya UKIMWI katika mkakakati wa haki za binadamu lenye makao yake mkabala na SIMEJ Hotel,mtaa wa Lubaga,kata ya Lubaga katika manispaa ya Shinyanga-picha na Kadama Malunde
Wafanyakazi wa shirika la AGAPE mkoa wa Shinyanga wakijitambulisha kwenye mkutano mkuu wa mwaka leo,aliyeshikilia kipaza sauti ni afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka Shirika hilo la AGAPE Deozawadi Marandu-picha na Kadama Malunde |
Afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka Shirika hilo la AGAPE Deozawadi Marandu akizungumza katika mkutano huo uliokutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka halmashauri ya wilaya ya Kishapu,wilaya ya Shinyanga na manispaa ya Shinyanga-picha na Kadama Malunde
Wadau wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini-picha na Kadama Malunde
Mkutano unaendelea-picha na Kadama Malunde
Akina mama kutoka Chibe katika manispaa ya Shinyanga wakiimba nyimbo kuhusu ukatili wa kijinsia-picha na Kadama Malunde |
Mkurugenzi wa shirika la AGAPE mkoa wa Shinyanga John Myola akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema mkoa wa Shinyanga umekithiri kwa matukio ya watoto kuachishwa masomo na kupewa ujauzito na ndoa za utotoni.Alisema kila siku watoto 16 wanabakwa mkoani Shinyanga na wengine 500 kila mwaka wanapewa mimba na kuolewa wakiwa na umri chini ya miaka 18-picha na Kadama Malunde