ANGALIA PICHA-TUKIO KUBWA LILILOTOKEA WILAYANI KISHAPU

Hapa ni pale palikuwa kijiji cha Kishapu kilichopo kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga,kijiji ambacho pamoja na vingine 7 vimevunjwa na kupewa  hadhi ya kuwa mamlaka ya Mji Mdogo wa  Kishapu baada ya mchakato huo kuchukua muda wa miaka 10 ili kukamilika.Pichani katikati ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akiweka jiwe la uzinduzi wa mamlaka ya Mji mdogo wa Kishapu.Uzinduzi huo uliofanyika jana ulienda sanjari na sherehe ya kuipongeza halmashauri ya wilaya ya Kishapu kufanya vizuri katika mbio za mwenge mwaka huu katika kanda ya Kwanza inayoundwa na halmashauri zaidi ya 40,wilaya hiyo imekuwa ya kwanza na ya pili kitaifa ikiongozwa na Kinondoni-Picha na Kadama Malunde
 Mkuu wa mkoa akifungua bango linalosomeka "Karibu mamlaka ya mji mdogo wa Kishapu"-Picha na Kadama Malunde
 Karibu Mamlaka ya mji mdogo wa Kishapu.Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kishapu la terehe 24 Oktoba mwaka 2008 liliridhia uanzishwaji wa mamlaka hiyo na kufuta vijiji vinane  ambavyo ni Mhunze,Kishapu,Mwanuru,Migunga,Mwataga,Lubaga Mwamagembe na Isoso, kabla ya kuvifuta mwaka 2009 na kupata vitongoji 56-Picha na Kadama Malunde
Wakazi wa Kishapu wakiwa katika viwanja vya Shirecu wakati wa sherehe kuipongeza wilaya ya Kishapu,kufanya vizuri katika mbio za mwenge mwaka 2014.Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi wa serikali,vyama vya siasa,waandishi wa habari na wananchi-Picha na Kadama Malunde

Wanakwaya kutoka Mamlaka ya mji Mdogo wa Kishapu wakifanya yao na wimbo wao unaopinga mambo ya rushwa-Picha na Kadama Malunde

Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinajiri uwanjani-Picha na Kadama Malunde

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akiwasalimia wakazi wa Mamlaka ya mji Mdogo wa Kishapu ambapo aliipongeza serikali inayoongozwa na rais Jakaya Kikwete kusikia kilio cha wanakishapu ya kutaka kuwa na mamlaka ya mji-Picha na Kadama Malunde

Kaimu mtendaji wa mamlaka hiyo mpya Phares Mahushi akisoma risala ambapo alisema mamlaka ya mji mdogo wa Kishapu inaundwa na kata ya Kishapu na Mwataga ikiwa na wakazi 19,347-Picha na Kadama Malunde

 Kikundi cha burudani cha ngoma ya Makhirikhiri 1 kutoka Kishapu kikifanya mambo wakati wa sherehe hizo-Picha na Kadama Malunde
 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga bi Annarose Nyamubi akishuhudia burudani na kushangazwa na jinsi vijana wa Makhirikhiri wanavyocheza utafikiri Makhirikhiri kutoka Botswana-Picha na Kadama Malunde
Makhirikhiri 1 wakifanya yao-Picha na Kadama Malunde

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku uvumilivu ulimshinda akaamua kucheza ngoma ya Makhirikhiri 2,ilikuwa ni shiiidah!!-Picha na Kadama Malunde

Uwanjani kulikuwa na zoezi la kukabidhi vyeti kwa watu wote waliofanikisha ama waliowezesha halmashauri ya wilaya ya Kishapu kufanya vizuri kwenye mwenge wa uhuru mwaka huu na kushika nafasi ya kwanza kikanda na nafasi ya pili kitaifa.Pichani ni kaimu mtendaji wa mamlaka ya mji mdogo wa Kishapu Phares Mahushi akiwa ameshikilia cheti chake-Picha na Kadama Malunde

 Mratibu wa mbio za mwenge bwana Godfrey Kajia akijiandaa kukabidhiwa cheti kwa kufanikisha mbio za mwenge mkoani humo na kuifanya Kishapu kuwa kinara kikanda-Picha na Kadama Malunde
Vyeti vinaendelea kukabidhiwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga-Picha na Kadama Malunde

Zoezi la kukabidhi vyeti linaendelea-Picha na Kadama Malunde

Na waandishi wa habari wamo,japokuwa wahusika wameona waandishi wa habari wa Televisheni tu(Star tv na Tbc),vyombo vingine mfano radio,magazeti na hata mtandao huu wa malunde1 blog ulioripoti matukio yote ya mbio za mwenge mkoa mzima  wa Shinyanga vikapotezewa!!.Pichani ni bwana Shaban Alley wa STAR TV akikabidhiwa cheti chake-Picha na Kadama Malunde

Mwandishi wa Tbc Greyson Kakuru akishikana mkono na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga kabla ya kukabidhiwa cheti chake-Picha na Kadama Malunde

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Khambaku akipokea cheti-Picha na Kadama Malunde

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga akipokea cheti kwa niaba ya CCM mkoa -Picha na Kadama Malunde

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akikabidhiwa cheti pia-Picha na Kadama Malunde

Sherehe hizo zilimalizika kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga kupewa zawadi ya ng'ombe wawili (jike na dume) na wazee wa Kishapu-Picha na Kadama Malunde

Mkuu wa mkoa akiwa anajiandaa kuondoka na ng'ombe wake-Picha na Kadama Malunde

Madiwani wa Kishapu wakiwa na mkuu wa wilaya ya Kishapu jukwaani-Picha na Kadama Malunde

<<BONYEZA MANENO HAYA USHUHUDIE MWENYEWE SHUGHULI ZA MWENGE WA UHURU MWAKA 2014 WILAYANI KISHAPU HATIMAYE WAMEPATA USHINDI >>

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post