Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA- TUKIO LILILOTIA FORA KATIKA MJI WA ISAKA HUKO KAHAMA

Hapa ni katika kijiji cha Isaka Stesheni kata ya Isaka katika halmashauri ya wilaya ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga,pichani wakazi wa kata hiyo wakiwa wamekaa chini ya mti wa mwembe kushuhudia tukio la kukabidhiwa mifuko 80 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho ikiwa ni sehemu ya ahadi zilizotolewa na wadau wa maendeleo wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa zahanati hiyo mwezi Mei mwaka huu.Mgeni rasmi  jana Jumapili alikuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja-Picha na Kadama Malunde

Aliyesimama ni mwenyekiti wa CCM kata ya Isaka akifungua mkutano wa hadhara wa mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja(Kulia),ambao ulihudhuriwa pia na mbunge wa jimbo la Msalala mheshimiwa Ezekiel Maige(kushoto).Mkutano huo ulienda sambamba na zoezi la kukabidhi mifuko ya 80 ya saruji na kukabidhi pesa shilingi 150,000/= na mipira 18 timu zote za kata katika jimbo hilo-Picha na Kadama Malunde

Aliyeshikilia kipaza sauti ni  katibu wa CCM wilaya ya Kahama ndugu Alexandrina Mahirane akiwasalimia wakazi wa Isaka-Picha na Kadama Malunde

Wakazi wa Isaka wakiwa wamenyoosha mikono kuunga mkono kilichokuwa kinajiri eneo la mkutano-Picha na Kadama Malunde

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Mabala Mlolwa akizungumza na wananchi wa Isaka,ambapo alisema wamefika mahali hapo ili kutekeleza ilani ya CCM na kwamba pamoja na kujenga zahanati bado wanaendelea kutekeleza miradi mingine ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara na muda sio mrefu ahadi ya rais Kikwete kuhusu huduma ya maji itaanza kutekelezwa-Picha na Kadama Malunde

Mbunge wa Jimbo la Msalala mheshimiwa Ezekiel Maige akizungumza na wakazi wa Isaka ambapoa aliwataka viongozi na wananchi kuungana pamoja katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwani mbunge imara anayeweza kazi yupo pamoja nao.Maige alitumia fursa hiyo kumpongeza mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja kutumia muda wake mwingi kujenga chama,pia kuwa kweli katika kutekeleza ahadi zake mfano tukio la kukabidhi mifuko 80 ya saruji ilikuwa ahadi iliyotolewa mwezi Mei 2014 na imetekelezwa-Picha na Kadama Malunde

Mbunge huyo wa Msalala Ezekiel Maige hakusita kusema kuhusu nia yake ya kuendelea kuwatumikia wakazi wa Msalala kwani ndiyo nyumbani na kwamba ana uchungu wa kuwaletea maendeleo wananchi wake.Alisema hata suala ya kupatikana kwa halmashauri ya Msalala linatokana na mchango wake.Aidha alisema mchakato unaoendelea hivi sasa ni kuhakikisha Isaka inakuwa Mamlaka ya Mji mdogo wa Isaka-Picha na Kadama Malunde

Wananchi wakimsikiliza mbunge wao,ambaye aliwaahidi kuwa Radio ya ISAKA itakayoanza kusikika hivi karibuni itakuwa kwa ajili ya watu wote (Radio ya Jamii) hivyo kuwaomba waitumie kwa maendeleo yao.Hata hivyo Maige hakusita kuzungumzia kuhusu jitihada alizofanya katika sekta ya elimu ambapo shule zote za sekondari zilizopo katika jimbo lake zina huduma ya Umeme na shule 5 za kata zina hostel(bweni) ili kuwafanya watoto wasome mahali salama/mazingira rafiki-Picha na Kadama Malunde

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akiwahutubia wakazi wa Isaka kabla ya kukabidhi mifuko ya saruji na zawadi kwa timu za mpira katika jimbo hilo.Mgeja alitumia fursa hiyo kuwatahadhalisha wananchi kuhusu UKAWA ambapoa alisema UKAWA ni "Umoja wa Kamati ya Watu Wachache",akiwa anamaanisha watu wachache wanaotaka kuharibu amani ya nchi kwa kuendekeza matusi na kubeza mafanikio yaliyofikiwa na CCM kupitia mwenyekiti wake rais Jakaya Kikwete-Picha na Kadama Malunde

Kulia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akikabidhi kwa kamati ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Isaka Stesheni mfuko wa saruji ukiwa ni miongoni mwa mifuko 80 iliyotolewa na mbunge wa Msalala Ezekiel Maige aliyetoa mifuko 50,mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi akiyetoa mifuko 20 na diwani wa kata ya Isaka Ibrahim Six Masanja aliyetoa mifuko 10 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi walizotoa mbele ya mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja wakati wa harambee iliyopatikana mwezi Mei mwaka huu katika kijiji hicho ambapo mamilioni ya pesa yalipatikana-Picha na Kadama Malunde

Kushoto ni diwani wa kata ya Isaka Ibrahim Six akikabidhi mfuko wa saruji kwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga kabla ya mwenyekiti kukabidhi kwa kamati ya ujenzi ya zahanati ya kijiji cha Isaka Stesheni-Picha na Kadama Malunde


 Kushoto ni mbunge wa Msalala Ezekiel Maige alikabidhi kwa mwenyekiti shilingi milioni 1.4 alizokuwa ameahidi kuzisaidia timu za mpira za kata katika jimbo lake wakati wa harambee iliyofanyika mwezi mei mwaka huu kijijini hapo-Picha na Kadama Malunde
 Kulia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga akihesabu pesa shilingi laki 5 zilizotolewa na diwani wa kata ya Isaka Ibrahim Six kuchangia timu za mpira katika kata yake -Picha na Kadama Malunde

Kushoto ni mbunge wa Msalala Ezekiel Maige akikabidhi mipira kwa niaba ya mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi( aliahidi kutoa mipira 18 wakati wa harambee ya kusaidia timu za mpira mwezi mei 2014).Baada ya mheshimiwa Maige kukabidhi mipira kwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja,mwenyekiti naye akigawa mipira hiyo kwa wahusika(Timu 14 za mpira wa miguu na timu moja mira wa pete ya kata ya Isaka-Picha na Kadama Malunde

Kushoto ni mmoja wa viongozi wa timu za mpira wa miguu akipokea shilingi laki 1 na nusu na mpira mmoja.Timu zote zilipokea shilingi 150,000/=na mpira mmoja zote zikiwa zimetolewa na wadau wa michezo mkoani Shinyanga wakiongozwa na mbunge wa Msalala Ezekiel Maige.
Mipira ilikuwa 18 ilibaki miwili ambayo ilikuwa zawadi kwa msindi wa mechi iliyofanyika kijijini hapo kati ya Isaka Stars na Home Boys ambapo mshindi alikuwa Isaka star aliyeibamiza Home Boys bao 1-0
Timu zilizopewa zawadi ni Isaka Star,Home Boys,Rege Star,Mwakata Star,Pembe la ng’ombe ,Isaka Ntungulu,Nhumbi,Mwashigini,Ulubalo,Buyozi,Jembe la Show,Chipukizi,Mwabayanda na Veteran Isaka huku timu ya mpira wa pete ya Isaka
 

-Picha na Kadama Malunde

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com