Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA ZA MWANAFUNZI ALIYEFARIKI AKIJIANDAA KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE HUKO SIMIYU,MAZISHI YATAFANYIKA KESHO

Mwanafunzi Yunis Festo enzi za uhai wake.Hii picha marehemu aliipiga tarehe 1,Novemba 2014 siku ya mahafali ya shule ya sekondari Simba wa Yuda-Picha na Damian Kageba Lupimo
Mwili wa marehemu ukiwekwa kwenye gari kwa ajili ya kusafirishwa  jana jioni tayari kwa mazishi kesho Jumatano huko Kwimba mkoani Mwanza-Picha na Damian Kageba Lupimo

Mwili wa marehemu ukiwa kwenye gari jana jioni-Picha na Damian Kageba Lupimo

Walimu wakiwa kwenye gari wakisafirisha mwili wa marehemu-Picha na Damian Kageba Lupimo

Wanafunzi na walimu wa Shule ya sekondari Simba wa Yuda wakiwa shuleni jana jioni-Picha na Damian Kageba Lupimo
 Mazishi ya mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la Yunis Festo aliyekuwa anasoma kidato cha nne katika shule ya sekondari Simba wa Yuda iliyoko katika kijiji cha Bulima wilaya ya Busega yanatarajia kufanyika kesho huko Kwimba mkoani Mwanza .

Mwili wa marehemu umesafirishwa jana jioni kutoka shuleni

Yunis Festo aliyezaliwa tarehe 26.02.1996 amefariki dunia jana saa 11 alfajiri  zikiwa zimesalia saa chache  tu kuanza kufanyika kwa mtihani wa kidato cha Nne kote nchini ulioanza jana Jumatatu.

Malunde1 blog imeambiwa kuwa mwanafunzi huyo amefariki dunia jana baada ya kukimbizwa  katika kituo cha afya  Bulima na wanafunzi wenzake aliokuwa nao bwenini alipozidiwa majira ya saa 9 usiku wa kuamkia jana.

Habari zinasema kuwa mwanafunzi huyo alikuwa anaumwa kichwa na kwamba alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Sickle Cell.

Malunde1 blog inawapa pole ndugu,jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huo.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Yunis Festo.Amina

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com