Hiace yenye namba za usajili T761 CKD ikiwa imepinduka baada
kuparamia tuta la barabarani na kupoteza mwelekeo kisha kutumbukia mtaroni katika
eneo la Buhangija mjini Shinyanga barabara ya Tinde-Shinyanga leo saa nne na nusu asubuhi-Picha na Kadama Malunde
Gari hilo likiwa limeharibika vibaya-Picha na Kadama Malunde
Mashuhuda wakiongea na waandishi wa habari,ambapo walisema dereva alikuwa anafukuza na hiace nyingine huku akipisha gari jingine alipofika kwenye tuta gari ikamshinda,ikapinduka mara 3,ikagonga daraja kisha kutumbukia mtaroni-Picha na Kadama Malunde
Kaimu Mganga
mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Mfaume Salum akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema wamepokea miili mitano ya watu waliofariki
dunia papo hapo eneo la tukio na wengine walifariki wakati wakipatiwa matibabu
katika hospitali hiyo na kwamba majeruhi 9 wanaendelea kupatiwa matibabu-Picha na Kadama Malunde
Ndani ya wodi namba 5 walikolazwa baadhi ya majeruhi.Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Longinus Tibishubwamu anasema watu waliopoteza maisha ni 9,majeruhi ni 9-Picha na Kadama Malunde
Majeruhi akipatiwa matibabu-Picha na Kadama Malunde
Majeruhi akiwa wodini akipatiwa matibabu-Picha na Kadama Malunde
Majeruhi Emmanuel John aliyekuwa anatoka Mwakitolyo
kwenda Mwanza na gari hiyo iliyokuwa inaishia mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde
Majeruhi Katumbi Nangi akiwa nje ya wodi namba 5 aliyekuwa
anasafiri kutoka Ulowa akizungumza na waandishi wa habari-Picha na Kadama Malunde
Majeruhi akiwa ndani ya wodi namba 7,hatukupata jina lake-Picha na Kadama Malunde
Majeruhi
Flora Ngudungi aliyekuwa anasafiri kutoka Kahama kwenda mjini Shinyanga akiwa
amelazwa katika wodi namba 7 katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga-Picha na Kadama Malunde
Majeruhi akiwa wodini(hatukupata jina lake)-Picha na Kadama Malunde
Social Plugin