Waziri wa Maadili wa Uganda Simon Lokodo ameagiza kukamatwa kwa msanii Franklin kutoka Nigeria ambaye anatuhumiwa kwa kusambaza picha za utupu alizopiga akiwa na mpenzi wake Desire Luzinda.
Serikali ya Uganda ilipitisha sheria ya ‘Anti-ponography’ ambapo kusambaa kwa picha hizo kunamtia hatiani jamaa huyo kwa kuvunja sheria hiyo,iwapo atakutwa na hatia adhabu yake ni faini ya milioni 50 za Uganda sawa na dola elfu 20 ambazo ni zaidi ya milioni 30 za Kitanzania au kifungo cha miaka 10.
Franklin anatafutwa kwa kuvujisha picha hizo ambapo inasemekana kuvunjika kwa uhusiano wao kumepelekea jamaa huyo kuvujisha picha hizo.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com