Mwanafunzi Yunis Festo enzi za uhai wake.Hii picha marehemu aliipiga tarehe 1,Novemba 2014 siku ya mahafali yake katika shule ya sekondari Simba wa Yuda |
Habari tulizozipata kutoka mkoani Simiyu ni kwamba mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la Yunis Festo aliyekuwa anasoma kidato cha nne katika shule ya sekondari Simba wa Yuda iliyoko katika kijiji cha Bulima wilaya ya Busega amefariki dunia .
Yunis Festo aliyezaliwa tarehe 26.02.1996 amefariki dunia saa 11 alfajiri ya leo zikiwa zimesalia saa chache tu kuanza kufanyika kwa mtihani wa kidato cha Nne kote nchini ulioanza leo.
Mdau wa Malunde1 blog bwana Damian Kageba Lupimo aliyeko eneo la tukio anasema mwanafunzi huyo amefariki dunia alfajiri ya leo saa 11 baada ya kukimbizwa katika kituo cha afya Bulima na wanafunzi wenzake aliokuwa nao bwenini alipozidiwa majira ya saa 9 usiku wa kuamkia leo.
Habari zinasema kuwa mwanafunzi huyo alikuwa anaumwa kichwa na kwamba alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Sickle Cell.
Damian Kageba Lupimo anasema pamoja na wanafunzi wengine wa kidato cha nne katika shule hiyo kuendelea na mitihani yao kama kawaida lakini hali ya majonzi imetawala katika shule hiyo.
Social Plugin