Huyu ni msichana ambaye juzi alikutwa katika uchochoro wa bar ya Galax mjini Kahama mkoani Shinyanga majira ya saa 12 asubuhi akiwa hajitambui kutokana na kile kinachodaiwa kuleweshwa pombe na watu wasiojulikana huku nguo zake zikiwa zimechana chanwa
Baadhi ya wananchi wakimuangalia binti huyo akiwa hana fahamu huku akiwa katika kichochoro huku nguo zake zikiwa zimechanwa na watu wasiofamika mjini Kahama.
Askari polisi wa kituo cha polisi Kahama Thomas Munyongo akijaribu kumtambua msichana huyo na bila mafanikio na kuomba msaada katika kituo cha polisi .
Baadhi ya watu wakijaribu kumtambua msichana huyo ingawa baadaye alijulikana kwa jina moja la Pili .
Baadhi ya wananchi wakimchukua binti huyo kwenda kwenye gari ya polisi na kupelekwa hospitali ya wilaya ya Kahama .
Hivi ndivyo msichana alipochukuliwa kupelekwa hospitali ya wilaya kahama kwa uchunguzi zaidi
Baadhi ya askari polisi wamtoa msichana ndani ya gari ya polisi baada ya kumfikisha hospitali ya wilaya ya Kahama
Daktari akijaribu kumkagua kama yuko hai .
Hivi karibuni mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya alipinga marufuku biashara ya ngono katika wilaya yake,kutokana wasichana wengi kufanya biashara hiyo haramu .
Aidha wilaya kahama imekuwa ni sehemu kubwa kwa wasichana kuingia katika biashara ya ukahaba jambo ambalo linafanya wasichana wengi kubakwa na kutupwa katika mitalo ya maji au manyumba yasio kwisha .
Social Plugin