Habari zilizotufikia hivi punde katika chumba cha habari cha Malunde1 blog ni kwamba basi la Musoma Express lenye namba za usajili T138 BDQ likitokea Dar es salaam kwenda Musoma limepata ajali katika eneo la Usanda hatua chache baada ya kutoka katika mzani wa Tinde barabara ya Tinde Shinyanga,usiku huu.
Inaelezwa kuwa wakati dereva akiendesha basi hilo ghafla mwanamme mmoja(mtembea kwa miguu) alikatisha barabarani na kusababisha ajali hiyo.
Inaelezwa kuwa basi hilo limeharibika na kwamba mtu aliyegongwa na basi hilo amefariki dunia papo hapo.
<<SOMA HABARI ZAIDI HAPA>>
Social Plugin