![]() Picha ya basi hilo baada ya ajali |
Habari zilizotufikia hivi punde kutoka mjini Kahama ni kwamba Basi la Wibonela Express likitoka Kahama mkoani Shinyanga kwenda jijini Dar es salaam limepata ajali asubuhi hii katika eneo la Phantom. Ajali hiyo imetokea leo saa 12 asubuhi katika eneo la Phantom kilomita chache kutoka Stand ya Mabasi mjini Kahama baada ya basi aina ya Scania lenye namba za usajili T 412 CGN mali ya Wibonela ambalo lilikuwa likitokea mjini Kahama kwenda jijini Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka. Mwandishi wa Malunde1 blog Ndalike Sonda kutoka Kahama anasema ajali hiyo imetokea asubuhi hii baada ya basi hilo kumshinda dereva katika kona ya Phantom na kusababisha aruke kutoka kwenye basi hilo la kufanya basi hilo lipinduke. Habari zinasema kuwa watu watu wanne akiwemo mtoto mmoja,wanaume wawili na mwanamke mmoja na watu zaidi ya 40 kujeruhiwa. Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa ajili ya matibabu.
Uongozi wa hospitali ya wilaya ya Kahama umesema waliofariki dunia ni watu wanne majeruhi 41
BONYEZA MANENO HAYA KUONA MAJINA YA WALIOPOTEZA NA MAISHA NA MAJERUHI <<ANGALIA PICHA ZA AJALI HIYO HAPA CHINI>> |
Social Plugin