Vuta nikuvute kuhusu sakata la pesa za Escrow imetokea na kusababisha Bunge la Tanzania kuvunjika usiku huu wakati likiendelea na mjadala wa kashfa ya Escrow, baada ya wabunge kushindwa kukubaliana njia sahihi ya kuwawajibisha baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaotuhumiwa kuhusika na sakata la wizi wa pesa hizo.
Bunge hilo, leo limeweka rekodi ya kuwa na mjadala wa muda mrefu Zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Hadi kufikia kuvunjika kwa kikao hicho ilikuwa ni saa 4.(30-45)usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Hatua hiyo kwa namna flani iliamsha hisia tofauti kutoka upande wa kambi ya upinzani pamoja na wajumbe wa kamati ya hesabu za Serikali ambao walitishia kutoka nje hadi viongozi wanaodaiwa kulindwa na bunge hilo wawajibike wenyewe.
Ilikuwa saa tano kasoro ambapo kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, mh. Freeman Mbowe alisimama na kumtuhumu Spika wa bunge kuwakumbatia wezi wa Pesa za Escrow, hali iliyowafaya wabunge wa upinzani wasimame na kuanza kuimba nyimbo za kuwataka wezi watoke ndani ya ukumbi wa bunge...
Wabunge wa upinzani waliokuwa wanaungwa mkono na baadhi ya wabunge wa CCM walidai kiti kinaonekana kuwa na maamuzi tayari kuwalinda wanaotuhumiwa kuhusiana na Sakata la Tegeta Escrow Account (Hasa Prof. Muhongo)
Hali hiyo ilisababisha baadhi ya wabunge kuanza kupiga kelele na kuimba bungeni,huku wengine wakinyanyuka kwenye viti vyao na kutoka nje.
Spika amelazimika kuahirisha bunge hadi watakaposhauriana na Bunge hilo linategemewa kuendelea na kikao chake hapo kesho.
Spika wa Bunge hilo Anne Makinda karibu muda wote wa kikao hicho alijikuta akitoa tahadhari kwa wabunge wake kujilinda na hatua za kuingilia mihimili mingine ya utawala ya Tanzania ambayo ni Mahakama na Serikali.
HEBU PITIA KIDOGO YALIYOJIRI KIKAO CHA BUNGE CHA LEO JIONI( Kwa Mujibu wa Jamii Forums) KUANZIA MWANZO HADI BUNGE LINAAHIRISHWA USIKU HUU
DONDOO MUHIMU KIKAO CHA JIONI
Kigwangalla: Sijawahi kuona Profesa muongo kama MuhongoKigwangalla: Toka lini pesa za watu binafsi zikawekwa Benki Kuu?
Mpina: Ni bahati mbaya tuna Profesa muongo kama Muhongo ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini
Mpina: Pesa zilizotolewa hazijalipwa kwa mmiliki halali wa IPTL, PAP sio wamiliki halali!
Mpina: Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliingilia majukumu ya TRA ktk kukusanya kodi
Zitto: Nimekuwa na mgogoro na chama changu lkn kwenye hili wameniunga mkono, kwa mara ya kwanza nimehudhuria kikao cha UKAWA
Zitto: Kuna baadhi ya wajumbe wanadai tumetumwa na Uingereza. Hakuna kinachonituma kufanya haya, ni uzalendo kwa nchi yangu
Zitto: Mahakama ilikiri kuwa kweli tulikuwa overcharged; ikaamriwa yafanywe mahesabu upya!
Zitto: Prof. Muhongo alisema anaheshimu mahakama za ndani. Jaji utamwa hakuwa anaamua kesi ya Escrow wala Capacity Charges
Zitto: Jaji hakusema kokote kuwa toeni hela mkawape IPTL. Hakuna sehemu alikotaja kitu kama hicho
Zitto: Kama TANESCO ina madeni makubwa na haina hela; Tanzania ina deni kiasi gani la Taifa? Basi tumeshauzwa!
Zitto: Muhongo alikuta TANESCO ikiwa na hasara ya Bil 43. Sasa TANESCO ina deni la zaidi mara 4!
Zitto: TRA wamegundua fraud kwamba nyaraka za PAP zilikuwa forged! Nchemba ameonesha ukomavu ktk hili
Zitto: Hivi watanzania tumefikia hatua ya kuukata utanzania kabisakabisa?
Zitto: Prof. Muhongo anadai yeye hahusiki na mambo ya makampuni. Sheria iliyotungwa mwaka 2012 haisemi hivyo!
Umeme umekatika Bungeni, wabunge wanashangilia!
Zitto: Kijana aliyesema Singh ni tapeli ametengenezewa kesi ya mauaji. Alifukuzwa kazi! Naomba apatiwe ulinzi
Zitto: Prof. Tibaijuka aliniandikia mchango wake wa maandishi kuelezea alivyopata fedha; tunawaachua Kamati ya Maadili
Zitto: System ili-collapse wakati wa mchakato wa uhamishaji wa mabilioni haya
Zitto: Tuhuma zikiachwa bila kufanyiwa uchunguzi watu huziamini. Naomba tuhuma za Lusinde kwangu zifanyiwe uchunguzi
Zitto: Naomba wanaonishughulikia wanishughulikie mimi; mwacheni mamangu apumzike (anatokwa machozi)
Kafulila: Tusiache kujadili kifo cha Waziri Mgimwa kisa mwanae hataki; kuna siku Rais atakufa na mwanae atataka tusichunguze
Chenge: Naomba neno KUFA listumike bali litumike neno KUFARIKI linakuwa na staha kidogo
Pendekezo la Serikali kumkamata Harbinder Singh Sethi kwa money laundering limekataliwa na Serikali hadi kesi iliyopo iishe
Lissu: Sethi akamatwe. Shauri lililopo mahakamani ni shauri la baadae! Akamatwe kwa sababu jinai kubwa imefanyika
Lissu: Pendekezo hili la serikali naomba wabunge wasilikubali; mtu huyu ahukumiwe kwa jinai
Simbachawene anapendekeza Sethi asikamatwe kama ilivyopendelezwa na Serikali; wabunge wanazomea
Mdee: Si ajabu kwa mtu mmoja kuwa na kesi ya jinai na kesi ya madai. Huyu Sethi afunguliwe kesi ya jinai
Halima Mdee: Kilicholetwa na Serikali ni ovyo, kinalinda wezi (kutaka Sethi asikamatwe mara moja)
Pindi Chana: Wa kukamatwa si Sethi peke yake; vyombo vya dola vifanye uchunguzi kwanza kubaini jinai iliyofanywa
Zitto: PCCB na TRA wameshafanya uchunguzi; mnataka vyombo gani vingine vifanye uchunguzi?
Werema: Eneo hili ndo litaleta mgongano mkubwa kati ya Bunge na Mahakama. Kwa sasa ni vigumu kusema "mkamate"
Makinda: Mnaposema akamatwe mnakosea, sisi siyo mahakama, tutafute njia nyingine na tuweke lugha ya kwetu siyo ya mahakama
==================
MAAZIMIO
Pendekezo la kwanza la kumkamata na kumfilisi bwana Seth lina marekebisho ya serikali, naibu waziri wa Sheria anasema haiwezekani
Pendekezo la pili kuhusu Rugemalira, serikali imeweka marekebisho kuhusu uhalali wa pesa za Rugemalira alizogawa
Azimio la TATU limerekebishwa kuwa waliopokea pesa wachunguzwe na kuchukuliwa hatua mahususi kwa mujibu wa sheria
Pendekezo la NNE. Kamati inazitaka mamlaka kuzitangaza benki za Mkombozi na Stanbic kama asasi za utakatishaji fedha
Azimio la 4 limepita kwamba Kamati inazitaka mamlaka husika ikiwemo benki kuu kuchukua hatua dhidi ya benki zote zilizohusika
Azimio la TANO: Serikali ipitie upya mikataba yote ya umeme na kutoa taarifa kabla ya kumalizika kwa Bunge la bajeti lijalo
Azimio la SITA: kuhusu Bodi ya TANESCO kuvunjwa kwa kusababisha pesa kuchotwa na hasara, serikali imekataa, mjadala unaendelea
Kingwangala: Kanuni zetu zinataka mtu yoyote anayetaka mabadiliko ya maazimio lazima awe amekawasilisha kabla
Kafulila: Kwa mujibu wa mkataba wa IPTL, maamuzi ya mwisho yanafanywa na mahakama ya London, bodi walikuwa na maamuzi hayo na haikuwajibika na maamuzi ya mahakama za ndani ya nchi
Majibu: ISCD ilisharidhia injuction ya mahakama ya Tanzania na ikaijulisha standard charted hivyo si sahihi kusema ISCD ina mamlaka ya mwisho, IPTL pia ilipata injuction kwenye mahakama za Tanzania
IPTL sio kampuni ya kimataifa tena bali kampuni ya ndani
Mdee: Bodi ya TANESCO, napendekeza vyombo vinavyohusika vifanye uchunguzi vitendo vya jinai na kuchukua hatua kwa bodi ya TANESCO
Mbowe: Kazi yote hii pengine tusingefika hapa kama bodi ingekua makini, bodi ya TANESCO haiwezi kukwepa lawama hii. Bodi ya TANESCO iwajibishwe
Lissu: Maneno ya Mdee yanahusu jinai, ishu ni bodi ya TANESCO, (Anapendekeza bunge livunje bodi ya TANESCO ivunjwe na iundwe upya kuongeze ufanisi.
Shekifu: Tusifike mahala bunge likatoa amri lakini kutekeleza shughuli pia tuna mihimili mitatu, bunge linaishauri tu serikali na bunge haliwezi kuivunja bodi ya TANESCO
Azimio hili ni la bunge hivyo tuepuke kuvunja katiba
Zitto: Bunge linaelekeza kwamba bodi ya TENESCO liundwe upya maana taasisi zote zimeshachunguza kama TAKUKURU na nyinginezo
Maelekezo ya Lissu yanapitishwa na wabunge
Azimio la Saba: Kamati imethibitisha katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini amefanya uzembe pia amesaidia pesa za Escrow akaunti kulipwa kwa asiyestahili, kamati inashauri uteuzi wake utenguliwe mara moja.
Waziri: Maswala yote yatachukuliwa hatua baada ya uchunguzi.
Kafulila: Halina mabadiliko na kama ni uchunguzi umeshafanywa na CAG na TAKUKURU, bunge kama chombo kinachoisamamia serikali libaki na meno yake ya kuisamamia serikali.
Simbachawene: Katibu mkuu ni mtumishi wa umma, na mwenye mamlaka nae ni raisi wa jamhuri hivyo bunge haliwezi.
Nagu: Nakubalianana uzito wa jambo, watendaji wa serikali wanawajibika kweli lakini wana haki zao, mamlaka husika waangalie na wachukue hatua.
Sendeka: Kamati inapendekeza uteuzi utenguliwe na TAKUKURU wamfikisha mahakamani, sisi tumeshauri na watu ambao tuna mamlaka nao ni waziri mkuu na raisi.
Zitto: Taarifa kwa waziri, taarifa hii inaweza kutumiwa na vyombo vya sheria.
Sakaya: Sio ikithibitika kwani kwa taarifa zilizopo imeshabitika
Suzan Lymo: Kwa uchunguzi ambao umeshafanyika, katibu mkuu huyu ana matatizo kwa sababu PAC na CAG ameshaonyesha
Vyombo vya kiuchunguzi viendelee kufanye uchunguzi
Lissu: Bunge litofautishe maswala la kijinai na mendine sio ya kijinai kama kutengua uteuzi. Wapo wanaolindwa na sheria, lakini wapo wanaoserve kwa mamlaka ya raisi hauwezi ukasema wana protection ya kisheria. Tunaomba nipendekeze bunge linaazima na sio kupendekeza.
Zitto anapendekeza katibu mkuu asimamishwe kupisha uchunguzi.
Wasira: Lazima tukubali nchi inaendeshwa na mihimili mitatu, juzi tulipata tatizo la mahakama kuzuia bunge na sisi pia bunge tusiingilie serikali.
Mchangiaji: Uchunguzi utafanyikaje wakati watu wako kazini?
Werema: Mimi ndiye niliyemshauri Katibu Mkuu Maswi kushughulikia fedha, ninambeba hivyo shughulikeni na mimi
Imeshindikana kupita kwa azimio la saba, Spika kaamua waendelee na azimio la nane, watarudi kupiga kura mwishoni.
Azimio la nane: Bunge limemuondoa Naibu Waziri wa Nishati Masele kwenye mapendekezo kwa kuwa hana hatia ya kuadhibiwa
Azimio la tisa: Linajadiliwa kuhusu kutengua uteuzi wa Waziri Prof Muhongo lakini upande wa serikali imekataa
Bunge halina mamlaka ya kumwambia raisi atengue baada ya Lissu kulitaka bunge kutengua uwaziri wa Muhongo.
Mbaruku: Bunge kazi yake ni kushauri na bunge haliwezi kuwa messenger. (Anashauri anavyoona)
Muhongo ameshutumiwa amedanganya bunge lakini hamna popote iliposemwa fedha hizi ni za umma moja kwa moja. Hivyo nashauri versin ya muheshimiwa Chenge.
Shaha: Tunachohitaji ni lugha nzuri bila kudharau muhimili mwingine. Tuhoji na tumalize na tuulize wanaoafiki Lissu au Chenge.
Zitto: Akili yangu imechoka kidogo hivyo sina pendekezo.
Mbowe: Bunge kufikisha saa tano kasoro ni historia, lakini leo kuna uzito wa kiti na uzito wa wabunge kwa mamlaka ambayo yako ndani yao. Panaonekana kuna maamuzi mengine ya kulinda watu. Kwa nini leo tuna kigugumizi. Tunapata wakati mgumu kuendelea kushiriki kikao cha kulindana. Kwanini mnalinda wezi.
Baadhi ya wabunge wanasema wezi waondoke...
Sendeka: Naomba tukae na tujenge hoja, (Kelele zinaendelea)
SPIKA ANAAHIRISHA KIKAO CHA BUNGE MPAKA WASHAURIANE TENA(Spika aahirisha kikao cha Bunge ghafla baada ya kutokea sintofahamu baada ya Wapinzani kudai Waziri Muhongo analindwa )