BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU TUNAPOZIWEKA |
Hiace iliyopata ajali ikiwa eneo la tukio huku ikiwa
imeharibika vibaya
|
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio
|
Gari ikiondolewa eneo la tukio
|
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Dkt Anselm Tarimo akiwa na maafisa wa polisi mkoa wa Shinyanga eneo la tukio-Picha na Kadama Malunde |
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio
|
Watu tisa wamepoteza maisha leo majira ya saa nne na nusu asubuhi baada ya gari
ndogo Hiace yenye namba za usajili T761 CKD ikitoka Kahama kwenda Shinyanga
Mjini kupinduka katika eneo la Kona ya Buhangija mjini Shinyanga barabara ya Tinde-Shinyanga.
Walioshuhudia wanasema hiace hiyo ilikuwa katika mwendo
kasi ikifukuzana na Hiace nyingine ndipo ikamshinda dereva wake baada ya kupiga
Bamz ya Buhangija na kupinduka mara tatu kisha kutumbukia mtaroni.
Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema wameondoa miili mitano
ya marehemu katika gari hiyo.
Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa
Shinyanga na wanaendelea na matibabu.
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Mfaume Salum amesema wamepokea miili mitano ya marehemu,na wengine wamefariki dunia wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali hiyo
SOMA HABARI KAMILI HAPA
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Mfaume Salum amesema wamepokea miili mitano ya marehemu,na wengine wamefariki dunia wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali hiyo
Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SSP Longinus Tibishubwamu abiria waliofariki ni 9 na majeruhi wako 9.
Amesema gari lililopata ajali ni mali ya Fabian Mzaya wa Shinyanga ilikuwa ikiendeshwa na Anuari Awadhi mkazi wa wa Shinyanga aliyekimbia baada ya ajali kutokea
SOMA HABARI KAMILI HAPA