UNYAMA!! POLISI WAPIGA MWANANCHI KAMA MBWA MWIZI,YUKO HOI WODINI,WASINGIZIA KAPIGWA NA WANANCHI HUKO SIMIYU

Kijana Bundu Kibela(25) akiwa hoi katika hospitali ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu baada ya kupigwa na polisi
Kijana Bundu Kibela(25) akiwa hoi katika hospitali ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu baada ya kupigwa na polisi

Mwandishi wa Habari Samwel Mwanga kutoka Simiyu katika ukurasa wake wa Facebook ameandika yafuatayo:POLISI MASWA LAWAMANI.
Jeshi la Polisi wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu linalalamikiwa kwa kitendo cha askari wake wawili wenye vyeo vya Police Constebo kumpatia kipigo kijana,Bundu Kibela(25)(pichani)bila ya kuwa na kosa na sasa amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Maswa Wodi namba 1.

Kijana huyo hali si nzuri haongei anakula kwa mrija na haja ndogo anatumia mrija.

Askari hao walikuwa doria siku ya tarehe 22/11/2014 majira ya 1:30 jioni eneo la soko la jioni karibu na mashine ya M
safiri.

Askari hao walikuwa wanne wakike(WP'S wawili)na wa kiume wawili.

Ila mashuhuda walisema kuwa WP'S hawakuhusika kumpiga.

Baadaye walitumia gari la kiraia kumkimbiza hospitali lakini wakatoa taarifa ya uongo kwa OCD kuwa kijana huyo amepigwa na wananchi wenye hasira kali.

Tukio hili limefanyika machoni pa watu na kilichowaokoa askari hao wasipate mkong'oto kutoka kwa wananchi ni bunduki mbili SMG walizokuwa nazo vinginevyo tungesema mambo mengine.

Vitendo hivi ndivyo vinavyowafanya wananchi walichukie jeshi la Polisi.
RPC Simiyu na OCD Maswa chukueni hatua.IGP Mangu hakuna haja ya kuwa na askari wa namna hiyo.Askari wenye tabia ya Upolisi wa kizamani wa kupiga raia hovyo hovyo haikubaliki kabisa.Tusilee uozo.
BOFYA HAPA KWA HABARI NA VISA VYA MAPENZI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post