Ustadh Khalid Mwarangi, Imam wa Masjid Bilal ulioko mtaa wa Maranza, wilaya ya Likoni,Mkoa wa pwani kaunti ya mombasa nchini Kenya ameuawa kwa kupigwa risasi na watu waliokuwa katika pikipiki usiku huu.
Katibu wa mtaa wa Maranza, Kassim Mwamgula amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kueleza kuwa Ustadh Mwarangi amekufa alipokuwa wanampeleka katika hospitali ya wilaya ya Likoni.
Mwamgula ameeleza kuwa watu wawili waliokuwa katika pikipiki walimlenga risasi marehemu alipokuwa akielekea msikitini wakati wa swala ya Isha.
"Mwanzo kulipita landcruiser ya polisi baadaye kidogo watu waliokuwa na pikipiki walifika wakageuza pikipiki wakampiga risasi" amesema Mwamgula.
Social Plugin