Pichani ni Mzee Warioba akitolewa nje baada ya vurugu zilizojitokeza katika Mdahalo wa "Mchakato wa Katiba Mpya, Maoni ya Wananchi na Katiba Inayopendekezwa" yaliyofanyika mapema leo hii Ubungo Plaza.
VURUGU zilizoambatana na ngumi kurushwa zimetokea hivi punde katika Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba alipokuwa akitoa mada kwenye mdahalo wa kujadili umuhimu wa kuielewa kwa kina Katiba inayopendekezwa kama ilivyopitishwa na Bunge Maalum la Katiba.
Inaelezwa kuwa vurugu hizo zimezuka baada ya watu waliokuwa na mabango kuvamia ukumbuni hapo na kusababisha baadhi ya watu waliokuwa wanafuatilia mdahalo huo kuwakabili na kuwapa kichapo.
Baada ya vurugu hizo, mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kurushwa moja kwa moja na ITV umesimamishwa kwa muda.
Kilichosemwa na wana mtandao kufuatia tukio hilo
KUTOKA JAMII FORUMS
CCM waleta vurugu kwenye Kongamano la taasisi ya Mwalimu Nyerere, Makonda ahusishwa
Kweli mfa maji hutapatapa atimaye ccm waanza kulazimisha maoni yao
Kutoka kwa wadau wengine:
By
Haki sawa
Hao vijana wameandaliwa na Paul Makonda , juzi alikuwa Serena hoteli na hao waliokuwa na mabango, ni mkakati ili midahalo izuiliwe kuwa inaamsha hisia mbaya .
By
ocampo four
Tokea nizaliwe sijawai kukasirishwa na hili jambo la Makonda kumpiga na chupa Mzee Warioba. Ni utovu wa nidhamu, ni dharau, ni ujinga, ni utoto, ni ukora, ni u.p.mbavu, ni akili ndogo, ni kukosa hekima na misamiati ya namna hiyo kwa hili jambo la Makonda kumpiga na chupa mzee Warioba. Nilikuwepo kwenye eneo la tukio kwa macho yangu nikashuhudia Makonda akimpiga na chupa mzee Warioba, nimeumia sana sana. CCM lazima waruhusu mawazo mbadala ili kujenga Taifa na kamwe kundi moja lenye mawazo yanayofanana hauwezi kujenga Taifa, lazima kuwepo na mawazo huru kwa pande zote katika jamii.
Ila nasita kusema kama kweli Makonda katumwa na CCM inawezekana kabisa katumwa na Nape au Sita. Warioba ni Kiongozi mstaafu tena katumikia Tanzania kwa moyo wote hivyo vijana kukosa adamu mpaka kufikia hatua ya kumpiga na chupa ni ujinga wa hali ya juu na vijana wa pande zote lazima tukemee hili jambo. Jeshi la polisi tafadhali mlifanyie hili kazi, na Makonda naomba nikupe ujumbe kuwa vijana hatutakaa kimya lazima tutakufanya kwa njia yoyote ile uweze kumuomba Mzee Warioba radhi na taifa kwa ujumla, Leo umefanya kwa Warioba, Kesho utasita kufanya kwa Mwinyi au Malecela au Mkapa...
Nimeuzunishwa sana na hili jambo....Shame on you Makonda
Ocampo four
Maneno ya Butiku naomba kunukuu "Huu uhuni uliyofanywa na Makonda haukubaliki hata kidogo, kitendo cha kumpiga Warioba na chupa tunaomba serikali iliangalie jambo hili na pia kuhakikisha katika midahalo mingine huyu muhuni asiwepo, Asanteni" mwisho wa kunukuu.
Maneno ya Butiku baada ya kikao kuisha akiongea na vijana nje ya ubungo plaza
Naomba kunukuu "Kamwe vijana wa CCM msikubali kuchagua viongozi wanaomtuma Makonda kutenda haya, ni uhuni na ujinga wa hali ya juu" alipoulizwa ni nani wako nyuma ya Makonda, bila kusita akasema Membe na Sita
By
Komando Kipensi
Wadau nipo hapa hali ya hewa imechafuka baada ya vijana kuonyesha mabango katiba inayopendekezwa inafaaa
Baada ya tukio hilo vijana wengine ambao wanaona haifai wakawavamia hao wenye mabango kua katiba inafaa....
Wakati mvutano huo unaendelea yule mbunge wa bunge la katiba mwenye ulemavu wa macho nae kavamiwa akaanza kupigwa .......
Wakati haya yote yakiendelea Makonda poul alikua yupo pembeni, baada ya kuona vijana wakimpiga mlemavu akaamua kuingilia kumuokoa mlemavu wakati hayo yote yakiendelea warioba alikua ametoka ukumbini hivyo si sahihi kusema makonda kampiga na chupa warioba.. maana warioba na butiku walitolewa mapema vuguvugu lilipoanza... ocampo ufor wacha uongo ....
Kitendo cha makonda kutaka kumwokoa mlemavu vijana wakamvamia kuanza kumpiga pia makonda.....
Kwa hali ilivyo wanzalishi wa vurugu ni vijana waliwavamia walioweka mabango kusema katiba inafaa.... je wasingewavamia kuna athari gani kwa nini waliwazuia wakati ni haki yao ya msingi kuwakilisha mawazo yao kikatiba...
Je ni busara kumpiga mlemavu kwa kua alishiriki bunge la katiba.... vijana wanampiga mtu asie ona. Je makonda kuamlia ugonvi mlemavu asipigwe kosa lake lipi?
Taifa linaharibika vyama vinatugawa ukisema katiba nzuri wewe ccm ukisema mbaya we ukawa sio sahihi.....
Bado nipo ubungo unaweza niuliza lolote,,,,
Nimesikitika kumwona okampo ufoo akipotosha umma....kwa siasa za chuki
Mzee Warioba akitolewa nje baada ya Vurugu hizo
KUTOKA FACEBOOK
Hapa ni Paul Makonda akidaiwa kutaka kumpiga Mzee Warioba huku walinzi wakimuondoa Mzee Warioba na kumsukuma Makonda pembeni.
PAUL MAKONDA kipondo ulichopata leo iwe fundisho kwa vijana wenzako wa CCM wanaotumwa kuvuruga midahalo bahati yako ungekufa.. "Asiyefunzwa na mamae walimwengu watakufunza".
Social Plugin