Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HAYA NDIYO MAMBO 9 TUNAYO JIDANGANYA NA KUSHINDWA KULETA MABADILIKO KATIKA MAISHA YETU


1.     Mimi siyo yeye
Wengi wanajilinganisha na wengine kuwa mimi siwezi na Fulani ndiyo wakufanya anaweza. Jiulize kwanini Fulani anaweza mimi siwezi amini unaweza fanya.

2.   Nitafanya baadae
“Kuahilisha jambo lolote lile ni kuua malengo yako” Hivyo acha kuahilisha mambo unayotakiwa kufanya fanya na ulete mabadiliko katika jamii yko inayo kuzunguka .
3.   Nimeridhika na Maisha yangu /hapa nilipo
Kuridhika pale ulipo ni kuonyesha kuwa umekata tamaa na kutokuwa na uwezo wa kufikiria usiridhike kwa pale ulipo ongeza uwezo wa kufikiri zaidi kimaisha.
4.   Sio la mhimu
Huu ni uongo mkubwa tunajipandikizaga wengi huona kama mawazo yao siyo ya mhimu kila jambo ni la mhimu kwani hilohilo huweza kubadilisha maisha yako kwa kulifanyia kazi
5.    Naogopa Kushindwa
Kabla ya kufikiria kushindwa fikiria nikiweza Je? Wengi walio fanikiwa katika maisha yao sio kwamba hawakushindwa walishindwa lakini hawakukata tamaa walijaribu tena na tena mpaka wakaweza.
6.   Nataka kuendeshwa/kupelekwa
Usifikirie mtu aje akulazimishe/kuelekeza kufanya jambo fanya kwa usahihi wako. Wengi hatufanikiwi kutokana na mawazo ya watu kukwambia unaweza/huwezi jiendeshe mwenyewe.
7.    Staki Mabadiliko
Kuna watu hawataki mabadiliko katika maisha yao na hiki ndiyo kitu kinacho kufanya ushindwe kubadilika katika maisha yako mabadiliko ni mhimu na ni mazuri pia jifunze kutoka kwa watu leo na kesho wakuone tofauti.
8.   Sina Muda
Hili litakufanya ushindwe kubadilika wengi wetu tunajidai tupo Busy sana katika mambo Fulani kuna jambo unafikiria kulifanya lakini unajidanganya kuwa huna muda waweza ona jambo hilo hilo linaweza badilisha maisha yako mapaka ukashangaa.
9.   Bado Mdogo
Usijione mdogo katika kufanya mambo unaweza kuwa mdogo na ukafanya mambo mazuri zaidi kuliko mpaka watu wakakushangaa kwani kuwa mdogo ndiyo kuna kupa uwezo mkubwa wa kufikiri mambo na kuchanganua usisubiri fanya maamuzi yako .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com