Yule jamaa alevunja rekodi ya kutembea kwenye waya mwembamba wa umbali mrefu Marekani amerudia tena kuvunja rekodi hiyo hatari, safari hii ameivunja akiwa Chicago, Marekani ambapo kama kawaida yake katembea juu ya waya kwa umbali wa futi 543 kwa kutumia waya huku akiwa amefunga kitambaa machoni.
Ni mchezo hatari ambao hata yeye mwenyewe anasema hakuwahi kufanya mchezo wa hatari kama huu.
Daredevil Nik Wallenda alianza safari yake ya kutembea kwenye waya katika jengo la Marina City towers hadi upande wa pili kwenye jengo la Burnett na kutumia dakika 1 na sekunde 15 kutembea umbali wa futi 543 kuikamilisha safari hiyo.
Akisimulia baada ya kumaliza kutembea umbali huo, Nick amesema, “..Kulikuwa na upepo mkali uliokuwa ukinipiga usoni…”– Nick
Hizi ni baadhi ya picha na video wakati jamaa akikamilisha mchezo wake.
Social Plugin