Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KIBAKA MWENYE HIRIZI APEWA KICHAPO CHA MAANA AKIIBA BODABODA ZA WATEJA KWENYE KUMBI ZA STAREHE HUKO MOROGORO



Aziz ‘akitaitiwa’ baada ya kutaka kuiba Bodaboda.
Dustan Shekidele, Morogoro



JAMAA aliyetajwa kwa jina moja la Aziz, amenusa kifo laivu baada ya kupokea kipigo ‘hevi’ kisha kukamatwa akituhumiwa kwa wizi wa pikipiki almaarufu bodaboda Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, jamaa alikamatwa hivi karibuni usiku mnene akidaiwa kutaka kutekeleza uhalifu huo jirani na Kumbi za Starehe za Nyumbani Park na Samaki Sports zilizopo maeneo ya Kihonda mjini Morogoro.

Mwanahabari wetu, akiwa ndani ya moja ya kumbi hizo alitonywa kwamba nje Aziz alikuwa ‘ametaitiwa’ baada ya kunaswa akijaribu kuiba moja ya bodaboda zilizokuwa zimeegeshwa nje.


Ilidaiwa kwamba mabaunsa wa eneo hilo ndiyo waliomshtukia jamaa huyo ambapo raia wenye hasira kali walipomsachi walimkuta na hirizi hivyo wakataka kumuua kwa kipigo kikali kilichosababisha kuloa damu tepetepe ndani ya dakika sifuri.

...Wakizidi kumtaiti.
Shukrani kwa polisi waliokuwa doria ambao walifika mara moja na kumuokoa jamaa huyo akiwa hoi kisha kumpiga pingu na kumtupa ndani ya difenda.
Akizungumza na mwandishi, mmiliki wa kumbi hizo, Farida Mees Metlou alisema kwamba tukio hilo lilikuwa la mara ya pili kwa Aziz kukamatwa akijaribu kuwaibia wateja wake wanaofika mahali hapo kula bata na muziki unaoporomoshwa na Bendi ya Bikon Sound.
Akisihi kuachiwa baada ya kupewa kichapo kikali.

“Huyu Aziz anataka kuniharibia biashara, hii ni sehemu ya watu wastaarabu na ulinzi upo wa kutosha hivyo wateja hawatakiwi kuwa na hofu, lolote likitokea linadhibitiwa mara moja kama ulivyoona kwa kijana huyu,” alisema Farida kwa kujiamini.
Hata hivyo, baada ya upepo kutulia, askari waliondoka na Aziz kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya maelezo zaidi ili sheria ichukue mkondo wake.
Chanzo Global

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com