Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KOCHA WA MBEYA CITY ABWAGA MANYANGA,KISA TIMU KUFANYA MADUDU

Kocha Juma Mwambusi ameuandikia barua uongozi wa Mbeya City ya kubwaga manyanga kuinoa timu hiyo kwa kuchoshwa na kelele za shutuma dhidi yake.
Mbeya City imeanza vibaya Ligi Kuu Bara msimu huu kwani inashika mkia ikiwa na pointi tano baada ya kucheza michezo saba, imeshinda mmoja, imetoa sare miwili na kufungwa minne.
Kufanya vibaya kwa timu hiyo kumeibua maneno mengi hasa wakimtuhumu Mwambusi kuwa ameshindwa kazi na ndio sababu uwezo wa timu hiyo umeporomoka.
Kutokana na jambo hilo, kocha huyo wa zamani wa Prisons ameamua kuachia ngazi ili kuwapisha wengine baada ya kuchoshwa na maneno mengi yanayoelekezwa kwake.
Mwamabusi alisema jana kuwa ameamua kujiweka pembeni ili kuwapisha makocha wengine watakaoweza kuinoa timu hiyo na kuipa mafanikio.
“Maneno ni mengi sana baada ya matokeo haya na wengi wanaelekeza maneno haya kwangu kuwa sifai, mimi mkali, hivyo nimeona bora niwaachie timu yao ili kulinda heshima yangu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com