Mwanzilishi wa Kanisa la The Pool of Siloam, Nabii Eliya Adam amefariki dunia juzi mchana, muda mfupi baada ya kuwaeleza wasaidizi wake kuwa siku hiyo ndiyo ilikuwa ya mwisho kwake kuishi duniani.
Nabii huyo ilianzisha kanisa hilo mwaka 2003 katika eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam, baadaye kuenea mikoa mbalimbali nchini.
Akitoa taarifa za kifo cha Nabii Eliya, Kuhani kiongozi wa kanisa hilo, Miaka 1000 Eliya alisema kabla ya kifo chake, Nabii aliwaita na kuwaeleza mambo manne.
“Kwanza, alituambia amemaliza kazi ya kulijenga kanisa, pili akasema gari lake lipo tayari na litakuja kumchukua leo mchana (juzi mchana). Baada ya kufariki ndiyo tukajua kwamba alipotueleza gari linakuja kumfuata kumbe ni kifo,” alisema.
Alisema nabii pia aliwataka kuhakikisha wanajenga makanisa ya kutosha na kuwataka waumini wa kanisa hilo kukamilisha kila jambo walilopanga.
Alisema Nabii Eliya alikuwa na umri wa miaka 54 na ameacha mke na watoto wanne. Mazishi yatafanyika Jumapili.
via>>Mwananchi
Social Plugin