LEO NI KUMBUKUMBU YA MIAKA MIWILI TANGU KUFARIKI KWA ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI LA SHINYANGA ALOYSIUS BALINA



ASKOFU BALINA ENZI ZA UHAI WAKE
                                                          
Jimbo katoliki la Shinyanga leo linafanya kumbukumbu ya kuadhimisha miaka miwili toka kifo cha aliyekuwa askofu wa jimbo hilo mhashamu ALOYSIUS BALINA.


Askofu Balina alifariki tarehe Novemba 6, mwaka 2012 alipokuwa amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza akisumbuliwa na maradhi ya kansa ya ini.

Mazishi ya aliyekuwa Askofu wa jimbo Katoliki la Shinyanga marehemu Aloysius Balina yalifanyika katika Kanisa Kuu la Mama Mwenye Huruma la Ngokolo Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini,vyama vya siasa na serikali akiwemo rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Toka kufariki kwa askofu huyo mpaka sasa jimbo katoliki la Shinyanga halijapata askofu mwingine.
                              

Kufuatia kifo hicho Baba Mtakatifu Papa Benedicto wa 16,mwaka 2012 alimteua Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza Mhashamu Yuda Thadeus Ruwaichi kuwa msimamizi wa kitume wa Jimbo la Shinyanga ,mpaka atakapoteuliwa Askofu mwingine.

Na Veronica Natalis-Malunde1 Blog Shinyanga


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post