BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU TUNAPOZIWEKA
Mwili wa
mtoto Mack Johnson ukitolewa kwenye kisima cha maji na wananchi
waliofika eneo la tukio wakishirikiana na jeshi la wananchi na jeshi la zimamoto
na uokoaji. Mtoto huyo (5)alikuwa anasoma darasa la awali katika shule ya Sheer Bliss
amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye kisima cha maji chenye urefu wa futi
50 kilichopo eneo la shule mtaa wa Majengo Mapya katika manispaa ya Shinyanga.
Kisima
chenye urefu wa futi 50 ambapo mtoto Mack amefariki dunia baada ya
kutumbukia,ngazi mbili za jeshi la zimamoto pamoja na kuungwa pamoja lakini
hazikuweza kufikia kina cha kisima hicho na badala yake ikatumika kamba ndefu
na mmoja wa wananchi kujitoa mhanga kutumbukia nayo kisimani kuutoa mwili wa
mtoto huyo.
Mashuhuda wamesema tukio hilo limetokea leo saa tatu asubuhi ambapo mtoto huyo alitumbukia
kwenye kisima hicho wakati akicheza na wenzake karibu na kisima hicho kilichopo eneo la shule ambacho
kimefunikwa na makaravati yaliyoonekana kuchakaa.
Kamba ikiwa ndani ya kisima ikiwa imeshikiliwa kwa nje na wananchi huku ndani akiwemo mmoja wa wananchi hao aliyeingia na kamba hiyo kuokoa maisha ya mtoto ndani ya kisima.
Katibu
tawala wa mkoa wa Shinyanga aliyekuwa eneo la tukio Dkt Anselm Tarimo amesema wamebaini kuwa mazingira ya shule hiyo siyo
rafiki, shimo lilikuwa halijafunikwa hivyo kuwaomba wataalam mbalimbali wawe
wanapita katika maeneo wanakosomea watoto ili kujua mazingira ya watoto
kuepusha majanga yanayoepukika.
BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU TUNAPOZIWEKA |