Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha |
Mtoto aitwaye
Paschal Bundala mwenye umri wa miaka 7 mkazi wa
kata ya Mwakitolyo wilaya ya Shinyanga vijijini amefariki dunia baada ya
kutumbukia kwenye dimbwi la maji.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga
Justus Kamugisha amesema tukio hilo limetokea Novemba 15 mwaka huu ambapo mtoto
huyo alifariki dunia papo hapo baada ya kutumbukia kwenye dimbwi hilo akichunga
ng’ombe.
Amesema chanzo cha tukio hilo ni mtoto huyo kuteleza na
kutumbukia kwenye dimbwi hilo.
Social Plugin