Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Nyandoto Wilayani Tarime Peter Mwikabwe mwenye miaka19 amekutwa amekufa kwa kujinyonga kwa kamba nyumbani kwao baada ya kuzuiwa kuuza ng’ombe wa baba yake .
Baba wa mwanafunzi huyo alisema mtoto wake alikwenda kwa ndugu yake na kumdanganya kuwa ametumwa achukue ng’ombe amuuze kwa ajili ya mahitaji ya shule lakini kabla hajapewa ngo’ombe hao walipiga simu nyumbani kwao kutaka kupata ukweli ndipo ikagundulika alidanganya na kunyimwa.
Baada ya kumkataza kutaka kuuza ngo’mbe kijana wake aliingia chumbani na walidhani amekwenda kulala lakini baada ya kimya cha muda mrefu waliingia chumbani kwake na kumkuta ananing’inia na kamba akiwa tayari amefariki.
Kamanda wa Polisi Tarime Lazaro Mambosasa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiwaasa vijana kuachana na tabia za kukimbilia maisha ya starehe ambayo hayana faida kwao.
Social Plugin