NB-Picha haihusiani na habari hapa chini |
Polisi mkoani Tanga, inamshikilia mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Old Tanga (16), (jina linahifadhiwa) kwa tuhuma za kutaka kujiua kwa sumu baada ya jaribio la baba yake mdogo kumbaka kushindikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fraisser Kashai alisema mwanafunzi huyo alitaka kujiua juzi sasa tatu usiku katika eneo la Barabara ya 20, Mtaa wa Ngamiani.
Kamanda Kashai alisema binti huyo alikunywa sumu ya panya, ambayo hata hivyo ilishindwa kutekeleza kusudio lake la kujiua.
Kabla ya kuamua kunywa sumu hiyo, ilidaiwa kuwa binti alitaka kubakwa na baba yake mdogo, Richard Leonard (39), lakini ilishindikana baada ya majirani kusikia kelele za kuomba msaada kutoka kwenye chumba ambacho binti huyo alitaka kubakwa.
“Polisi ilitaarifiwa kwa kupigiwa simu na mmoja wa majirani, ambao walimkamata mtuhumiwa na kumweka chini ya ulinzi pamoja na binti huyo hadi polisi walipowasili,” alisema Kashai.
Kamanda Kashai alisema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha baba mdogo wa binti huyo kwa muda mrefu amedaiwa kumsumbua, kumdanganya na kumpa ahadi ya kumnunulia vitu mbalimbali kama nguo na chips ili apate kufanikisha mpango wake.
Na Salim Mohammed, Mwananchi
Social Plugin