Katibu wa Uhamasishaji Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda akionesha kwenye simu yake picha ya video iliyopigwa wakati wa vurugu zilizotokea wakati wa mdahalo wa kujadili rasimu ya Katiba inayopendekezwa, kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza jana, ambapo Makonda aliyedaiwa kumpiga aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Waziri Mkuu wa zamani Jaji mstaafu Joseph Warioba, amekanusha kumpiga leo katika mkutano wa waandishi wa habari, Dar es Salaam.
Pia Makonda amesema kuwa hawezi kabisa kudiriki kumpiga kwani anamheshimu kama babake mzazi.
Amesema kuwa hata leo asubuhi amezungumza na warioba kwenye simu kumjulia hali. Warioba naye amekanusha kupigwa na Makonda wala mtu yoyote kwenye vurugu hizo.
Makonda akisisitiza jambo katika mkutano huo ambapo pia aliwaambia kazi kubwa aliyoifanya wakati wa vurugu hizo, ni kumsaidia Warioba kutoka salama pamoja na Mwanasiasa mwenye ulemavu wa macho ambaye pia alikuwa anamuokoa ili asipatwe na dhahama hiyo.Makonda akiendelea kuelezea kuwa anasikitishwa na vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii iliyomzulia kwamba yeye ndieye aliyesababisha vurugu wakati siyo. Pia amelaani watu wote waliosababisha vurugu hizo kwamba kitendo hizho kinadhoofisha demokrasia nchini. Habari, picha na Richard Mwaikenda wa Kamanda wa Matukio blog