WADAU wa Soka Mkoani Geita wameliomba shirikisho la mpira wa miguu Tanzani (TFF) kutenga ligi maalumu kwa ajili ya timu za majeshi baada ya kutokea vurugu wakati wa mchezo kati ya Geita Gold Sport na Green Warriors ya Dar-es-salaam uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Waja.
Wakizungumza baada ya mchezo huo uliofanyika juzi wadau hao walisema kuna haja ya timu za majeshi kucheza wenyewe kwa wenyewe ili kuepusha vipigo na vurugu kwa raia kwani kila timu ya polisi au wanajeshi wanapokwenda lazima mchezo uishe kwa vurugu.
Maoni hayo yamekuja baada ya wachezaji wa timu ya Green Sport Club kutaka kumshushia kipigo kikali mwamuzi wa mechi hiyo Maulidi Mikalo kutoka Mkoa wa Tabora baada ya kufungwa goli la pili katika kipindi cha kwanza lillilofungwa na Venance Jonas, Dakika ya 13 kipindi cha kwanza
Jeshi la polisi (FFU)wakiwa na mabomu ya machozi pamoja na bunduki za moto waliokuwa wanalinda usalama katika viwanja hivyo waliamua kuingilia kati ugomvi huo kwa kumnusuru mwamuzi huyo asipate kipigo kutoka kwa wanajeshi hao.
Imeelezwa kuwa mwamuzi aliamua vibaya mchezo huo hivyo kuwepo kwa madai kuwa huenda alinunuliwa na Geita Gold Sport Club.
"Jamani sisi tutakuwa tumehujumiwa, huyu kocha atakuwa kanunuliwa kwani hatutendei haki atakuwa amepewa pesa nyingi ili atunyanyase, yeye hata akiona kosa la kwao anakaa kimya, lakini la kwetu anapiga kipenga", alisema Salum Dialo mwalimu wa timu ya jeshi.
Naye mwalimu wa Geita Sport Clabu Mrisho Chogo yeye alisema ameshinda kwa sababu alijiandaa na kuifundisha timu yake kwa umakini zaidi na hakuna aliyenunuliwa hata mwamuzi aliyekuja kuchezesha ni mara ya kwanza kufika Geita.
Baada ya malalamiko hayo waandishi waliamua kumsaka mwenyekiti wa Geita Gold Sport Club Salum Ali Kulunge ili kutaka kujibu tuhuma hizo ambapo alisema sio kweli.
timu hiyo ya wanajeshi wao ni wagomvi kila wanakokwenda hata wafungwe au wafunge lazima waanzishe fujo.
"Timu hizi za jeshi zinapokwenda kucheza ni matatizo makubwa,wao wafungwe au wasifungwe lazima waanzishe vurugu kwa kuwapiga wenzao mimi naomba (TFF) Iwatafutiwe Timu zao wawe wanacheza wenyewe kwa wenyewe alisema M/kiti wa Geita Gold Club"alisema Kulunge.
Timu ya Geita Gold Sport Club imeibuka kidedea kwa kuifunga Timu ya Green Warrios ya Dar –es-salaam mabao matatu (3) kwa moja (1), ambapo bao la kwanza lilifungwa na Venance Jonasi Dakika ya 13 kipindi cha kwanza na la pili Ali Hatibu alifunga goli la pili Dakika ya 23 kipindi cha kwanza na goli la tatu alifunga Amos Makule Dakika ya 66 kipindi cha pili.
Na Valence Robert-Malunde1 blog Geita