Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA 40- MAHAFALI YA SITA KIDATO CHA NNE 2014,KOM SEKONDARI YATIKISA MJI WA SHINYANGA,MAMIA WASHUHUDIA

Wahitimu 128 kutoka shule ya Sekondari KOM iliyopo eneo la Butengwa mjini Shinyanga,bara ya kuelekea Old Shinyanga wakiingia ukumbini leo kulikofanyika mahafali ya 6 ya shule hiyo siku chache tu baada ya kufanya mtihani wao wa kidato cha nne 2014.Mgeni rasmi alikuwa mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele ambaye pia ni naibu waziri wa madini,huku wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa ,serikali na siasa,wazazi,wageni waalikwa na watu mbalimbali wenye mapenzi mema wamehudhuria mahafali hayo-Picha na Kadama Malunde
Wahitimu kidao cha Nne 2014 katika shule ya sekondari Kom iliyopo mjini Shinyanga wakiingia kwa madaha ukumbini wakati mahafahali yao leo shuleni hapo-Picha Kadama Malunde
 Awali mgeni rasmi mheshimiwa Stephen Masele(kulia)  akitembelea maonesho na ujenzi wa madarasa mapya katika shule ya KOM Sekondari,aliyevaa suti katikati ni mkurugenzi wa shule hiyo ndugu Jackton Koyi,akisikiliza kilichokuwa kinazungumzwa na wanafunzi wake kwa mgeni rasmi-Picha na Kadama Malunde
Mgeni rasmi alikuwa mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele ambaye pia ni naibu waziri wa madini akiwapungia mkono mamia ya watu waliohudhuria mahafali ya 6 ya shule ya sekondari KOM,ambayo sasa ina jumla ya wanafunzi 522,walimu 22,wafanyakazi wasio walimu 17 huku ikijivunia utoaji wa elimu bora kwa vijana wote-Picha na Kadama Malunde

Viongozi mbalimbali akiwemo mgeni rasmi mheshimiwa Stephen Masele wakiwa jukwaa kuu leo wakati wa mahafali ya kidato cha nne shule ya Kom Sekondari -Picha na Kadama Malunde

Wazazi wa watoto wakiwa wamesimama ukumbini leo wakati wa mahafali katika shule ya sekondari KOM,mahafali ambayo yamekuwa kivutio kikubwa kwa wote waliohudhuria-Picha na Kadama Malunde

Baadhi ya wahitimu wakiwa ukumbini leo-picha na Kadama Malunde
Wahitimu kidato cha nne 2014 katika shule ya sekondari KOM walinyoosha mikono kuonesha uwepo wao ukumbini-Picha na Kadama Malunde

Mamia ya watu wakishuhudia mahafali ya 6 ya wanafunzi kidato cha nne katika shule ya sekondari KOM-Picha na Kadama Malunde
 
Mkuu wa shule ya KOM sekondari  Mwita Waryoba akizungumza wakati wa mahafali hayo leo ambapo pamoja na mambo mengine alisema wanafunzi wao wameonesha heshima/nidhamu kubwa kwa kipindi chote walichokuwa shuleni kwa muda wa miaka 4 na kutumia fursa hiyo kuwataka wakaoneshe nidhamu nzuri kwa wazazi wao pia-Picha na Kadama Malunde
Mamia ya wakazi wa Shinyanga na maeneo ya jirani walijitokeza katika mahafali hayo leo-Picha na Kadama Malunde

 Wawakilishi wa wanafunzi waliohitimu masomo yao ya kidato cha nne mwaka huu katika shule hiyo wakijindaa kukata keki ,kushoto ni PS wa shule hiyo akisimamia zoezi zima-Picha na Kadama Malunde
Wahitimu wakikabidhi keki kwa mgeni rasmi-Picha na Kadama Malunde

Wahitimu wakimlisha keki mkurugenzi wa shule ya KOM sekondari ndugu Jackton Koyi-Picha na Kadama Malunde

Burudani_Vijana wa KOM sekondari wakionesha mchezo wao wa ubunifu wa mavazi,kila mmoja alikuwa na vazi lake-picha na Kadama Malunde
Wanafunzi waliohitimu masomo yao,Harrieth Albano na Anselm Dundee wakisoma risala kwa mgeni rasmi ambapo pamoja na mambo mengine walisem miongoni mwa changamoto zilizopo shuleni hapo ni wanafunzi kuchelewa kufika shuleni  likizo ikiisha hali ambayo inaathiri masomo ya wanafunzi-Picha na Kadama Malunde

Burudani ilikuwepo_Queen Stars wakifanya yao.Takwimu zinaonesha kuwa  jumla ya wanafunzi 657 wamehitimu kidato cha nne katika shule ya KOM sekondari  kuanzia mwaka 2009-2013,kati yao 409 sawa na asilimia 62.25% ya wahitimu wote walichaguliwa kuendelea na na kidato cha tano,wengine waliobaki wengi wao wamechaguliwa kujiunga katika vyuo mbalimbali-Picha na Kadama Malunde

 Mkurugenzi wa Kom sekondari Jackton Koyi akizungumza katika mahafali hayo ambapo alisema wanafunzi waliohitimu walianza wakiwa 116 lakini wamehitimu 128 huku akieleza kuwa anategemea wote watajiunga na kidato cha tano mwakani.Alisema mwaka jana wahitimu walikuwa 138 waliojiunga kidato cha 5 ni 123-Picha na Kadama Malunde
 Burudani inaendelea_Kikundi cha sarakasi kikitoa burudani vijana wanarusha kama ndege-Picha na Kadama Malunde
Kundi la sarakasi kazini-Picha na Kadama Malunde

Mmoja wa vijana wa sarakasi akijindaa kupita ndani ya ringi inayowaka moto-Picha na Kadama Malunde
 Wanashuhudia burudani matata-Picha na Kadama Malunde
Vijana wa KOM seondari wakitoa burudani-Picha na Kadama Malunde

Takwimu zinaonesha kuwa  jumla ya wanafunzi 657 wamehitimu kidato cha nne katika shule ya KOM sekondari  kuanzia mwaka 2009-2013,kati yao 409 sawa na asilimia 62.25% ya wahitimu wote walichaguliwa kuendelea na na kidato cha tano,wengine waliobaki wengi wao wamechaguliwa kujiunga katika vyuo mbalimbali-Picha na Kadama Malunde

Wakali wengine_wanitwa "Best Dancers" wakitoa burudani -Picha na Kadama Malunde

Licha ya changamoto zilizopo shuleni hapo,maendeleo ya shule hiyo kitaaluma ni mazuri ya kuridhisha-Picha na Kadama Malunde

HARAMBEE YA UJENZI WA MAABARA YA JIOGRAFIA-wageni waalikwa wakichangia walichokuwa nacho kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa maabara ya jiografia katika shule harambee hiyo iliendeshwa na mgeni rasmi mheshimiwa Stephen Masele na kufanikisha kukusanya shilingi zaidi ya laki moja papo hapo,ahadi milioni 8,huku jumla kuu ikiwa ni zaidi ya milioni 9 na mifuko kadhaa ya saruji-Picha na Kadama Malunde

Akina mama wakichangia katika harambee hiyo-Picha na Kadama Malunde

 Akina Baba nao hawakuwa nyuma katika harambee hiyo-Picha na Kadama Malunde
 Mgeni rasmi akavutiwa na mtoto aliyejiunga kwenye kundi la wanaume kuchangia ujenzi wa maabara ya jiografia,akaamua kupiga naye picha-Picha na Kadama Malunde
Dj Dany akifanya yake wakati wa mahafali hayo leo-Picha na Kadama Malunde

ZOEZI LA UTOAJI VYETI_ Mgeni rasmi akitoa vyeti kwa wanafunzi magwiji/ wenye uwezo mkubwa katika masomo mbalimbali -Picha na Kadama Malunde

 Ugawaji vyeti kwa washindi wa masomo ukiendelea-Picha na Kadama Malunde
Ugawaji vyeti unaendelea-Picha na Kadama Malunde

Mgeni rasmi akiendelea kugawa vyeti kwa wanafunzi wenye uwezo mkubwa katika masomo yao-Picha na Kadama Malunde

Mwanafunzi aliyechukua cheti cha usafi akiwa na wazazi wake/huyu kavunja rekodi kwa usafi kapewa cheti na pesa-Picha na Kadama Malunde

Huyu mwanafunzi ni miongoni mwa wale wenye uwezo mkubwa darasani,kapewa cheti na pesa pia-Picha na Kadama Malunde

 Mmoja wanafunzi wenye akili zaidi darasani-Picha na Kadama Malunde
 Mgeni rasmi akiwa na wanafunzi washindi wa jumla katika masomo yao,wa kwanza na wa pili na wasichana,wanatisha katika masomo ya hisabati na physics,wameondoka na vyeti na kitita cha pesa-Picha na Kadama Malunde
 Wanafunzi tatu bora washindi wa jumla katika masomo yote wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na mkurugenzi wa shule ya KOM sekondari-Picha na Kadama Malunde

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com