Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Updates!! BASI LILILOPATA AJALI TINDE NI MUSOMA EXRESS LA DAR -MUSOMA,MTU MMOJA APOTEZA MAISHA

Bofya hapa ujiunge nasi tukutumie habari zetu zote pindi tu zinapotokea

Malunde1 blog imefuatilia kwa ukaribu zaidi kuhusu ajali ya Basi iliyotokea usiku huu saa 4,ambapo tumeelezwa kuwa basi lililopata ajali ni basi la Musoma Express lenye namba za usajili T138 BDQ lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Musoma.

Basi hilo limepata ajali katika eneo la Usanda hatua chache baada ya kutoka katika mzani wa Tinde barabara ya Tinde Shinyanga.

Inaelezwa kuwa wakati dereva akiendesha basi hilo ghafla mwanamme  mmoja anayedaiwa kuwa ni mzee (mtembea kwa miguu) alikatisha barabarani na kusababisha ajali hiyo.

Jeshi la polisi limefika katika eneo la ajali.

Malunde1 blog imezungumza na mmoja wa askari wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga aliyeko katika eneo la tukio,ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu yeye siyo msemaji, amesema mwanamme  aliyegongwa na gari hilo amefariki dunia papo hapo na kwamba abiria waliokuwa kwenye basi hilo wako salama(hakuna majeruhi wala waliopoteza maisha).

Walioshuhudia tukio hilo wameiambia malunde1 blog kuwa dereva wa basi hilo hakuwa katika mwendo kasi ndiyo maana hakujatokea majanga zaidi.

Tutawaletea taarifa kamili hapo baadaye endelea kutembelea Malunde1 blog,Fahari ya Shinyanga......
Bofya hapa ujiunge nasi tukutumie habari zetu zote pindi tu zinapotokea

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com