Siku tatu baada ya kutolewa taarifa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania kuhusiana na safari ya rais Dkt. Kikwete kwenda Marekani kwa ajili ya kupatiwa matibabu, ipo taarifa nyingine kuhusiana na President baada ya kutibiwa.
Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji wa tezi dume baada ya uchunguzi wa kidaktari kugundua ana tatizo hilo katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland Marekani.
Upasuaji huo umechukua saa moja na nusu na umefanyika salama na kwa mafanikio ambapo sasa hali ya Rais Kikwete inaendelea vizuri japo bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Saa chache zilizopita kupitia ukurasa wa Twitter wa Rais Kikwete (@jmkikwete) Ikulu wameandika >>> “08/11/2014 Mheshimiwa Rais Dkt Jakaya Kikwete alifanyiwa upasuaji wa Tezi Dume uliokamilika salama katika Hospitali ya John Hopkins. – Ikulu”
Tweet nyingine kwenye Twitter ya President ikasema >>> “Leo 09/11 Mheshimiwa Rais anaendelea vizuri na ameanza mazoezi, tutaendelea kuwajulisha maendeleo yake na tuungane katika kumuombea. – Ikulu”
08/11/2014 Mheshimiwa Rais Dkt Jakaya Kikwete alifanyiwa upasuaji wa Tezi Dume uliokamilika salama katika Hospitali ya John Hopkins. – Ikulu
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) November 9, 2014
Leo 09/11 Mheshimiwa Rais anaendelea vizuri na ameanza mazoezi. Tutaendelea kuwajulisha maendeleo yake na tuungane katika kumuombea. – Ikulu
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) November 9, 2014
Social Plugin