|
Maelfu ya wakazi wa mji wa Shinyanga na maeneo ya jirani waliojitokeza jioni ya leo katika viwanja vya mahakama ya mwanzo Nguzo nane mjini Shinyanga katika mkutano mkubwa wa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa ndugu Halima Mdee ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kawe.Pamoja na mambo mengine viongozi mbalimbali wa Chama hicho walisisitiza umuhimu wa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura na kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa Desemba 14,2014 huku wananchi wakishauriwa kuachana na propaganda za CCM ambayo imeshindwa kuwaondoa Watanzania katika umaskini,kila siku maisha yanazidi kuwa magumu-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Viongozi mbalimbali wa Chadema ngazi ya wilaya,mkoa na taifa wakiwa jukwaa kuu jioni ya leo mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga mjini Hassan Baruti akifungua mkutano leo mjini Shinyanga ambapo aliwaomba wananchi kuungana kwa pamoja ili kuing'oa CCM madarakani na kuwapuuza wanaohama chama kwani wanatumiwa na watu wasioitakia mema Chadema-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
Makamanda wakinong'ona jambo-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
|
Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Shinyanga Peter Machanga akiwasalimia wananchi wa Shinyanga huku akiwataka wakurugenzi wa wilaya kutoa vipeperushi kuhusu taratibu za uchaguzi wa serikali za mitaa-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Wananchi wakinyoosha mikono kufurahia hotuba za viongozi wa Chadema jioni ya leo-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Mbunge wa Maswa Mashariki Sylivester Kasulumbayi akiongea na wananchi wa Shinyanga leo-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
Maelfu ya wananchi wakifuatilia mkutano wa Chadema jioni leo mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
|
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga pia mwenyekiti wa baraza la wanawake Chadema mkoa wa Shinyanga,Rachel Mashishanga akikaribisha wageni wa kitaifa wakiongozwa na mwenyekiti wa BAWACHA taifa Halima Mdee.Mashishanga alisema pamoja na serikali kuwapa wakazi wa Shinyanga Waziri wa madini,Stephen Masele lakini mbunge huyo hana msaada wowote kwa wananchi huku akiwataka watu wa Shinyanga kubadilika na kuiunga mkono Chadema-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
Wakazi wa Shinyanga wakifuatilia mkutano wa Halima Mdee jioni ya leo-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
|
Naibu katibu mkuu BAWACHA taifa Kunti Yusuph aliwasalimia wakazi wa Shinyanga ambapo aliwataka kuungana na Chadema ili kutengeneza maisha ya sasa na ya vizazi vijavyo-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
Mkutano unaendelea-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Katibu mkuu BAWACHA taifa Grace Tendega akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo alisema viongozi wengi wa CCM wanajinufaisha wao na watoto wao huku watanzania wakiendelea kuteseka na maisha magumu.Alisem njia pekee ya kuiondoa CCM ni kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kupigia kura viongozi wa vyama vya upinzani.Lakini pia aliwakumbusha umuhimu wa kulinda kura zao ili zisiibiwe kama ilivyofanyika chaguzi zilizopita kwani hata mbunge wa Shinyanga Stephen Masele aliiba kura akashinda hivyo sasa wawe makini-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Wananchi wakifuatilia mkutano-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Makamu mwenyekiti BAWACHA taifa Hawa Waipunga akizungumza mjini Shinyanga ambapo aliwataka wananchi kuunga mkono kiongozi yeyote kutoka vyama vya upinzani (UKAWA) anayeonekana kukubalika katika jamii ili kuiondoa madarakani CCM-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema,pia mwenyekiti wa Bawacha mkoa wa Kilimanjaro pia mbunge wa viti maalum Chadema mkoa wa Kilimanjaro Grace Kiwelu akiwasalimia wakazi wa Shinyanga ambapo aliwataka wananchi kuendelea kuiunga mkono Chadema na UKAWA lakini akawakumbusha kuchangia chama hicho-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
|
Mwenyekiti wa BAWACHA taifa Halima Mdee akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapoa alisema kitendo cha CCM kuchakachua kura ulitokana na wananchi kutolinda kura zao na sasa wamejipanga vyema ili kuhakikisha kuwa wanaingia ikulu huku akilitaka jeshi la polisi kukaa pembeni ili waishughulikie ipasavyo CCM kwani imechoka na nchi imeuzwa imebaki listi tu.Mdee alitumia fursa hiyo kuwataka wasukuma/watu wa kanda ya ziwa ambao wapo zaidi ya milioni 8 kubadilika kwani wana utajiri wa kila aina ikiwemo migodi 7 mikubwa lakini ni maskini kutokana na kukumbatia serikali isiyojali wananchi wake-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
|
Mwenyekiti wa BAWACHA Halima Mdee akiwapokea wazee wawili walioamua kuokoka na kurudi Chadema kwa kile walichodai CCM kutojali wananchi.Mwenye shati la kitenge ni mzee Joseph Rweyemamu(58) aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji cha Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga kwa muda wa miaka 15,akifuatiwa na mzee Robert Ng'welo(66) aliyekuwa katibu mwenezi wa CCK mtaa wa Jikolile kata yaNdembezi-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga |
Mzee Robert Ng'welo akikabidhi kadi ya CCM kwa HaliamMdee na kupewa kadi ya CHADEMA jioni ya leo.Mdee alisema Chadema ni chama cha watanzania bila kujali huyu ni mzee au la!!-Picha na Kadama Malunde-Shinyanga
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin