Tarehe 01/11/2014 muda wa saa 07:45hrs katika center ya Mhunze tarafa ya Kishapu na Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kumetokea kifo cha mtu mmoja na watu watatu kujeruhiwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu kulipuka ndani ya gari.
Gari hilo ni lenye namba za usajili T. 848 AKA MITSHUBISH FUSSO likiendeshwa na Khalifa s/o Mussa 39, muhangaza wa Ngara ambalo lilitoka tarehe 31/10/14 saa 04:00 hrs mjini Ngara kuja Mkoa wa Shinyanga wilaya ya Kishapu kupakia shehena ya mtama kwa mfanyabiashara alitwaye Donard s/o Nzugula (49) mkazi wa Muhunze.
Inaelezwa kuwa wakati gari hilo likiwa limeegeshwa dukani kwa mfanyabiashara huyo ili kusubiri kupakia mzigo huo dereva alishuka kununua sigara maduka ya jirani akamwacha utingo wake ndani ya gari peke yake ambaye anaitwa Juma s/o Rashid 21-23, mkazi wa Ngara ambaye ni familia ya mwenye gari(aliyefariki dunia)
Baada ya muda mfupi kama dakika 15 hivi dereva alisikia mshindo mkubwa na alipokwenda kwenye gari alimkuta utingo wake ametupwa nje ya gari na akiwa amefariki mwili wake ukiwa na majeraha tumboni,mkono wa kushoto kiganja kimekatika,mkuu wa kulia kwenye paja ambalo limechimbika hadi kwenye mfupa, shingoni upande wa kushoto kuna shimo kubwa lililosababishwa na kitu chenye ncha kali.
Pia mfanyabiashara Donard Nzugirwa Mwalimu ambaye ameumia mkono wa kulia kwa kuchanwa chanwa na vipande vya chuma,amepelekwa hospitali ya mkoa kwa matibabu zaidi.
Wengine ni Maganga Pius (14 ), mkazi wa Kishapu ambaye amejeruhiwa paja la kushoto,mgongoni na mkono wa kushoto.
Seni Edward (25 ), ambaye amejeruhiwa bega la kushoto, majeruhi wote wametibiwa na kuruhusiwa.
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba linafanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba linafanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo
Social Plugin