UNAWAJUA WALIOKULA PESA ZA ESCROW? MAJINA YAO YAKO HAPA,WAANIKWA LIVE BUNGENI

BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU TUNAPOZIWEKA 



Katika kikao cha Bunge kilichokaa leo Novemba 26 Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe na Makamu wake Deo Filikunjombe waliwasilisha Ripoti ya ishu ya Escrow ambapo kama hukupata kusikiliza wakati Ripoti hiyo ikiwasilishwa hii ni sehemu ya uwasilishwaji wa Ripoti hiyo.
…Katika fedha ambazo zimelipwa kwa watu binafsi katika Benki hizi yapo majina ya viongoozi wa kisiasa, viongozi wa madhehebu ya dini, Majaji na watumishi wengine wa Serikali..“– Zitto Kabwe.
Kwa upande wa Viongozi wa Kisiasa walioingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mheshimiwa Andrew Chenge Mbunge, ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, shilingi Bil. 1.6,mheshimiwa Anna  Tibaijuka Mbunge na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, shilingi Bil. 1.6, Mheshimiwa William Ngeleja Mbunge na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini, shilingi milioni 40.4, ndugu Daniel Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini shilingi milioni 40.4, ndugu Paul Kimiti, ambaye ni Mbunge mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga shilingi milioni 40.4 na ndugu Enos Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7…“– Zitto Kabwe.

"Upande wa Majaji Prof. Eudes Ruhangisa, aliingiziwa milioni 404. na J.A.K Mujulizi aliingiziwa shilingi milioni 40.4, kwa upande wa Watumishi wa umma,Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa shilingi milioni 40.4,Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa shilingi milioni 40.4,Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8",Zitto Kabwe
"Viongozi wa Madhehebu ya Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu Methodius Kilaini shilingi milioni 80.9,Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4,Watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, mabox, magunia na lumbesa",Zitto Kabwe
… Kamati imependekeza kuwa uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali utenguliwe mara moja na kisha afikishwe Mahakamani kwa matumizi mabaya ya Ofisi yaliyopelekea Serikali kupoteza mabilioni ya fedha za umma…“– Deo Filikunjombe.
Kwa upande wa Waziri Mkuu kuhusiana na suala hili baada ya kupitia vielezo vilivyomo kwenye ripoti ya CAG kamati imejiridhisha pasipo mashaka kuwa Waziri Mkuu  alikuwa ana taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa kuchota  fedha kwenye akaunti ya Escrow, ushahidi ulioletwa mbele ya kamati  za ofisi ya CAG ulionyesha kuwa Waziri Mkuu alikuwa akipata taarifa juu ya jambo hili na kamati imethibitishwa kuona kuwa Waziri Mkuu hakuchukua hatua yoyote kuzuia muamala huu usifanyike…“– Deo Filikunjombe.
Kamati kwa kuzingatia kielelezo namba 22 inathibitisha kwamba bila shaka Waziri Mkuu alikuwa analijua jambo hili vizuri sana na kwamba aliridhia mhamala huu usifanyike, ndio maana katika maelezo yake  ya Bungeni mara kadhaa Waziri Mkuu alilithibitishia Bunge kuwa fedha za ESCROW hazikuwa fedha za umma…”– Deo Filikunjombe.
MSIKILIZE HAPA MHESHIMIWA ZITTO AKIWATAJA WALIOKULA PESA ,KISHA SIKILIZA MAPENDEKEZO YA KAMATI,FILIKUNJOME AKIWASILISHA,WANAOPASWA KUWAJIBIKA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post