Kama tulivyoawaahidi kuwaletea simulizi mbalimbali kuhusu kanda ya Ziwa Victoria,kupitia ukurasa/kipengele chetu kipya cha" UTAMADUNI LAKE ZONE",angalia juu kwenye blog,kila siku za Jumamosi ,leo Malunde1 blog inakuletea sehemu ya SITA ya simulizi ya kusisimua kuhusu Gamboshi
SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU GAMBOSHI SEHEMU YA 6
Mtunzi; Timotheo Mathias
MAZINGIRA; Shinyanga vijijini.
Simu yake-0765676242(WhatsApp)
timotheomathias0@gmail.com
Maana ya maneno yaliyotumika kwenye simulizi
-GAMBOSHI ni makazi au eneo linalotumika kuhifadhia misukule.
-MSUKULE ni mtu aliyechukuliwa kwa njia ya kishirikina (kichawi) akiwa mzima (hai), lakini kwa upeo wa kawaida ni dhahiri kuwa amekufa
Ilipoishia...........................
Kuna siku nikiwa nimekaa nimejiinamia nikiwaza yote yaliyotokea mkuu wa wachawi alinifuata na kunishika mkono na wote tukaanza kurudi kambini.
Tulipofika Sheila aliitwa na bibi mmoja pia na yeye aliitwa kwa mkuu, mkuu alimwambia bibi kuwa mwezi ujao ni sikukuu itakayofanyika nchini Nigeria, na huko zinahitajika nyama laini kama wanafunzi wa shule za msingi na baadhi ya walimu wao.
Nimekuchagulia vijana shupavu na imara utawatumia katika mashule huko vijijini kuleta wanafunzi.
Mkuu alipomaliza alitukabidhi mabegi yaliyosheheni pipi, biskuti na hela za sarafu, tayari kwa safari kwenda kuleta roho za watu kama tulivyoagizwa.
Mkuu alipomaliza alitukabidhi mabegi yaliyosheheni pipi, biskuti na hela za sarafu, tayari kwa safari kwenda kuleta roho za watu kama tulivyoagizwa.
Endelea sasa...............
Safari tuliianza kuelekea mashuleni hasa shule za vijijini, katika safari yetu tulikuwa watatu mimi na Sheila tukiwa tumebeba mabegi mgongoni.
Mbali na Sheila pia tulikuwa na bibi ambaye yeye aliteuliwa na mkuu kama kiongozi wetu lakini yeye alikuwa amening'iniza mfuko wa rambo mkononi.
Kipindi hicho cheo changu kiliianza kupanda hapo GAMBOSHI kwani tuliweza kukabidhiwa gari aina ya VX land cruiser nyeusi.
Safari yetu ilianza ikiwa bibi na dreva walikaa mbele ya gari, pia na sisi tulikuwa nyuma yao.
Kwa binadamu wa kawaida hawezi kuiona safari yetu ikiwemo gari, kwani barabara zetu zipo tofauti na barabara za kawaida .
Barabara zetu ni za kishirikina zaidi, kwani zinapenya/zinapita sehemu yoyote mfano, majini, mlimami, juu ya nyumba na pia gari yetu inauwezo wa kuingia ndani ya nyumba kupitia mlangoni.
Kila kijiji lazima kuna mwanachama wa wachawi, safari yetu tuliweza kufikia tamati kijiji tulichokisudia na tulifikia kwa mwachana wetu.
"Mpenzi msomaji wa simulizi hii kaa ukitambua fika ya kuwa CHAKULA KIKUU CHA WACHAWI NI NYAMA IKIWEMO NA YA BINADAMU"
Kweli tuliweza kufika na kukaribishwa vizuri, pia kwa macho ya kawaida tulionekana isipokuwa gari.
Mama wa familia akiwa na mume wake na watoto watatu walitukaribisha, upande wa mume alikuwa hajui chochote mambo ya kishirikina na pia alikuwa mchungaji wa kanisa.
Mama aliweza kututambulisha kwa mume wake, na mume wake alitukaribisha kwa furaha maana alimpenda sana mungu.
Baada ya hapo mama alitupeleka katika chumba cha wageni na kutuambia kuwa tukae kwa siku tatu, ya nne tuanze kazi iliyotupeleka.
Usiku ulipofika mama alituambia kuwa nyama ya kula kesho imeisha, kwa hivyo nilitakiwa kuamka usiku kwenda kuchukua nyama.
Kweli ilipofika usiku mama alikuja kuniamsha na kuniambia tuondoke haraka,lakini kabla hatujaondoka nilimuuliza vipi kuhusu mme wako?.
Mama alionekana kushtuka kidogo na kuniambia turudi chumbani kwake.
Tuiingia taratibu mpaka kitandani na kumkuta mme wake amelala, tulichokifanya mama alichukua dawa na kumuwekea mme wake puani.
Loo!! mume alipiga chafya na kugeukia upande wa pili na pembeni yake tuliweka gogo kama mke wake.
Nakumbuka ilikuwa usiku wa manane tuliweza kufika katika kaya moja ambayo walikuwa wafugaji wa mifugo, tulichokifanya kabla hatujaenda zizini tulizizungukia nyumba zote na kumwaga dawa juu ya paa.
Malengo ya kufanya hivyo ilikuwa ni kuwafanya wasisikie chochote kinachoendelea nje (walale fofo).
Tulifikia eneo la zizi na kuanza kutoa miti iliyotumika kufunga mlango kwa umakini mkubwa ikiwa mimi ndio kiongozi wa mambo.
Tuliweza kuingia zizini na kuchagua dume la kondoo lililonona, niliichinja humo humo ndani ya zizi na damu iliweza kutapakaa ndani ya zizi, baadae tukanyanyua na kupeleka nyumbani.
Kabla hatujaondoka tuliweza kuweka alama za nyayo ya fisi , ili kusudi wakiamka waamini kuwa aliwavamia fisi.
Baada ya siku tatu, ya nne mama aliweza kutupa majina ya wanafunzi wanaostahili kupelekwa GAMBOSHI kwa ajili ya kuliwa kwenye sherehe ya dunia iliyotarajiwa kufanyika nchini Nigeria.
Mama alitupa majina ya watu saba, watatu walikuwa wanafunzi, mmoja mwalimu na watatu ni vijana wa mitaani.
Mama alidai kuwa hao wote aliowachagua walikuwa wakiwaonea sana watoto wake bora wakaliwe nyama.
Tukiwa watatu mimi, Sheila na bibi tuliweza kufika shuleni.
Tulianza kumimina dawa kila nje ya milango ya madarasa na ya walimu.
Kipindi hicho hakuna aliyetuona.
Tukiwa tunamimina dawa nilishangaa kumuona bibi akianguka chini na kupiga kelele kama mtoto mdogo.
Hapo ndipo nilishuhudia wanafunzi wakipiga kelele na kushangilia huku wanatoka madarasani na kuelekea ofisini na wengine wakimzingira bibi.
Baada ya muda mfupi wanakijiji walijaa shuleni na kumuamuru bibi avue nguo, kweli alivua nguo zote na alibakia kama alivyozaliwa...
Itaendelea wiki ijayo siku ya Jumamosi kupitia www.malunde1.blogspot.com