Kama tulivyoawaahidi kuwaletea simulizi mbalimbali kuhusu kanda ya Ziwa Victoria,kupitia ukurasa/kipengele chetu kipya cha" UTAMADUNI LAKE ZONE",angalia juu kwenye blog,kila siku za Jumamosi ,leo Malunde1 blog inakuletea sehemu ya KUMI ya simulizi ya kusisimua kuhusu Gamboshi
SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU GAMBOSHI SEHEMU YA 10
Mtunzi; Timotheo Mathias
MAZINGIRA; Shinyanga vijijini.
Simu yake-0765676242(WhatsApp)
timotheomathias0@gmail.com
Maana ya maneno yaliyotumika kwenye simulizi
-GAMBOSHI ni makazi au eneo linalotumika kuhifadhia misukule.
-MSUKULE ni mtu aliyechukuliwa kwa njia ya kishirikina (kichawi) akiwa mzima (hai), lakini kwa upeo wa kawaida ni dhahiri kuwa amekufa
Ilipoishia.......................
Unaambiwa kutoka Tanzania mpaka Nigeria unatakiwa ufike ndani ya dakika 6, maana nyungo zimesetiwa hivyo, ukizidisha dakika 6 wewe itakuwa halali ya wananchi kutoka duniani.
Kipindi hicho mkojo ulikuwa umenibana sana ilinibidi nichomoke kimya kimya kwa kitendo cha haraka nilijificha nyuma ya msitu na kuanza kukojoa.
Nihisi kama kuna kitu kwa nyuma kinanigusa taratibu shingo niligeuka nilishtuka baada ya kumuona babu aliyegeuzwa kuwa kuku na mkuu wa wachawi yupo nyuma yangu,Duh nilitoa macho kama chura kabanwa mlango....
Endelea...................
Baada ya kugeuka na kumkuta ni babu nilimuuliza kulikoni? nikamwambia nataka nirudi nasubiriwa tuna safari ya kwenda Nigeria.
Kabla sijamalizia alinikatisha na kunishika mkono na kuniambia " Kijana wangu kwanza nakushukuru kwa kunielewa na kuiachia pete kwani ndiyo iliyonisaidia na mpaka unaniona tena.Safari yote nilikuwa naifahamu hii pete yako chukua itakulinda huko uendako nakutakia safari njema",alisema Babu.
Baada ya babu kunikabidhi pete na kuniachia mkono nilianza kuondoka, babu alinishika na kuniambia kuwa "usiwe na wasiwasi Sheila ni mzima na yupo kambini" nilimjibu asante na kuondoka kurudi kujumuika na mwenzangu.
********************
Tukiwa tumekaa kwenye nyungo zetu na kupanga mstari mmoja, mimi nikiwa wa pili kutoka mkono wa kushoto,Mkuu wa wachawi alibonyeza rimoti yake ya kisigino cha mguu wa binadamu na nyungo zetu taratibu zilianza kunyanyuka kwa kwenda juu (angani).
Nilibaki nashangaa baada ya wenzangu kuniacha kwa kasi, na ungo wangu ukiwa unaenda taratibu.
Pia na mimi nilikichukua kisigino changu na kukibonyeza na ungo wangu ulianza kuondoka kwa kasi ya ajabu unaambiwa kadri unavyozidi kubonyeza kisigino ndiyo kadri ungo unazidi kuongeza kasi ya kuondoka.
Nilikuwa peke yangu nyumakwani mwenzangu wote walikuwa mbele yangu, waliniacha kama mita 100.
Na katika maisha yangu nilikuwa sijawahi kupanda usafiri wenye kasi kama ungo tena kwa kutumia rimoti ya kisigino.
Nilizidi kuongeza kasi ya kubonyeza kisigino lakini haikuwa rahisi kuwapata wenzangu maana nyungo zilikuwa na kasi sawa.
Baada ya dakika mbili tukiwa angani kila mmoja wetu alionesha ujuzi wa kuutawala ungo wake na pia tulianza kuachana, mimi nilishika nafasi ya nne kati ya watu sita.
Nikiwa nafasi ya nne, nilimshuhudia mtu aliyekuwa akituongoza akipiga kelele na ungo wake ukaanza kuyumba hadi ungo ukafeli na kudondoka chini.
Hali khalika n aaliyekuwa anamfuatia alianza kuyumba lakini alikaa sawa hivyo niliitumia fursa hiyo kuwapita hadi kushika nafasi ya pili.
Baada ya dakika tano ungo wangu ulizidi kuwa mzito na ukibonyeza kisigino hakuna kilichobadilika, na baadaye nilianza kuona watu wengi sana kwa chini.
Na hatimaye ungo ulianza kuzunguka sehemu moja na baada ya muda mfupi ungo ulianza kutua taratibu hadi mpaka chini na mimi kutoka kwenye ungo na watu walitukaribisha kwa furaha.
Baada ya kutua kitu cha kwanza tulipewa damu ya binadamu kwenye kikombe, na kupewa wosia na zawadi tuliyoahidiwa.
Kwa vile mimi nilikuwa wa pili sikupewa zawadi ya aina yoyote na aliyekuwa wa kwanza aliweza kupandishwa cheo na kuwa kiongozi pia aliweza kutolewa kwenye kundi letu.
Watu wageni kutoka nchi mbalimbali tulikusanyika kwa pamoja na kuanza kupewa maagizo na kiongozi wa huko alisema "kazi kubwa iliyowaleta hapa ni sherehe pamoja na kupandishwa cheo lakini kabla hujapandishwa kuna jaribio utapewa na ukishafuzu moja kwa moja unapandishwa cheo"
******************
Tuligawanishwa katika makundi ya watu wanne wanne na kila kundi tulipewa mtihani tofauti, malengo yao ni kuleta damu ya binadamu.
Pia kila mmoja wetu alipewa nguvu za kichawi za kutosha.
Basi tukaingia mtaani kusaka damu za watu.
Tuliweza kwenda mpaka sehemu ya baharini ambapo tuliona boti moja katikati ya bahari iliyokuwa imebeba watu wapatao 12.
Tulikubaliana kwenda kuiteka hiyo boti ili kuweza kuleta damu zao.
Tuliizingira hiyo boti na kusimama katika pande nne za dunia na mikono yetu kuinyosha kuelekeza kwenye boti pia na nguvu za kichawi zikifanya kazi.
Boti ilianza kuyumba na taratibu boti ilianza kuzama majini pia na sisi tuliwahi kwa ajili ya kuchukua damu zao kabla hawajakata roho.
Tulifika katika boti ilikuwa ndani ya maji, pia tulifika wote katika boti na tulipoigusa ile boti nilishangaa kuona mwanga mweupe kama radi,ukatupiga na wote kwa pamoja tulirushwa juu na kila mmoja aliangukia sehemu yake na mmoja wetu aliweza kupoteza uhai...