|
Ndani ya ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kishapu_Awali kabla ya kwenda kufunga mafunzo ya ufyatuaji wa matofali kupitia mashine za kisasa katika kikundi cha vijana cha Isoso chenye vijana 40 katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.Mkuu wa wilaya hiyo Wilson Nkhambaku akizungumza wakati mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Jane Mutagurwa( wa tatu kutoka kulia)akiwasilisha taarifa juu ya wilaya hiyo kwa , wakati Meneja wa Shirika la nyumba la taifa(NHC),Mkoani Shinyanga Ramadhani Macha( wa kwanza kutoka kulia).
Mutagurwa alisema, halmashauri ya Kishapu ina uhaba wa nyumba za watumishi ,hata nyumba za kupanga kwa wananchi wilayani humo hakuna, hali ambayo inawalazimu baadhi ya watumishi wake kwenda kupanga mjini Shinyanga, jambo ambalo limekuwa changamoto kubwa katika halmashauri hiyo-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kishapu
|
|
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku(mwenye suti) akizungumza kwenye mradi wa matofali wa vijana wa Isoso wilayani Kishapu,ambao wamepatiwa mashine ya kufyatulia matofali na shirika la nyumba la taifa,na sasa vijana hao wamepatiwa mafunzo kuhusu namna ya kufyatua matofali yenye ubora .Nkhambaku alisema shirika la nyumba ya taifa, limegawa mashine za kisasa nne za matofali wilayani humo, ambapo kila kikundi cha vijana 40, kitakuwa na mashine moja, na mara baada ya kupewa mafunzo ya kuzitumia watakabidhiwa mashine yao, ikiwa ni pamoja na kupewa mitaji ya kujiendeleza-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kishapu |
Kulia mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu Jane Mutagurwa, akiwa katika eneo la mradi wa matofali wa vijana 40 wa Isoso,katikati ni Meneja wa Shirika la nyumba la taifa(NHC),Mkoani Shinyanga Ramadhani Macha akishuhudia kazi iliyofanywa na vijana wa Isoso.Meneja wa Shirika la nyumba la taifa mkoani Shinyanga Ramadhani Macha, alisema shirika hilo linatarajia kujenga nyumba hamsini wilayani humo, zoezi lake litaanza mwezi Januari mwaka 2015) ambapo hadi kufikia Oktoba nyumba hizo zitakuwa zimekamilika na hivyo kuondoa changamoto ya uhaba wa nyumba za watumishi wilayani Kishapu-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kishapu
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akiangalia moja ya matofali yaliyofyatuliwa na vijana wa Isoso baada ya kupewa mafunzo juu ya namna ya kufyatua matofali yenye ubora unaotakiwa-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kishapu
|
Baadhi ya wanakikundi cha Isoso wakiwa eneo la mradi
Lengo la serikali kupitia Shirika hilo la nyumba ya taifa (NHC), ni kuhakikisha vijana hawakai vijiweni na kulalamika hakuna ajira, bali watumie fursa hiyo kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kishapu
|
|
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akichanganya udongo ili afyatue matofali-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kishapu |
|
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akijiandaa kukabidhi mashine ya kufyatulia matofali kwa vijana hao ili waanze kufanya kazi rasmi baada ya kuhitimu mafunzo yao na kuanza kujiingia kipato kupitia kazi hiyo katika kukabiliana na umaskini-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kishapu |
|
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku akikabidhi mashine iliyotolewa na shirika la nyumba la taifa kwa vijana hao.Akifunga mafunzo hayo na kukabidhi mashine hiyo Nkhambaku aliwataka vijana hao, kuitumia mashine hiyo ipasavyo kwa madhumuni yaliyokusudiwa na kuendeleza kikundi chao, hali ambayo itawaondoa katika janga la umaskini pamoja na kujenga nyumba zilizo bora na kuondokana na nyumba za tembe-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kishapu |
|
Namna tofali zinavyoatkiwa kupangwa wakati wa ujenzi-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kishapu |
|
Wanakikundi cha Muungano cha wajasiriamali kutoka Kishapu wakionesha bidhaa zao za asili ikiwemo mikeka wanayotengeneza kwa mikono yao ili kuingiza kipato-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kishapu |
Mkurugenzi wa halmashauri ya Kishapu Jane Mutagurwa akingalia moja ya bidhaa inayotengezwa na akina mama wajasiriamali kutoka Kishapu-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kishapu
|
Mwanakikundi akionesha bidhaa yake-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kishapu |
|
Akina mama wajasiriamali kutoka Kishapu-Picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Kishapu |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com