BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU TUNAPOZIWEKA
Ni mabingwa katika kuwa na nywele zilizotengezwa vizuri ama hata ufugaji wa ndevu.
Lakini afisa moja wa soka nchini Uturuki yuko katika harakati ya kupiga marufuku mpango huo.
Ilhan Vacvac,mwenyekiti wa kilabu ya Uturuki ya Genclerbirligi ametangza vita dhidi ya wanasoka wanaovuga ndevu.
Jambo la kushangaza ni kwamba yeye mwenyewe anafuga masharubu.
Amesema kwamba mchezaji yeyote atakayekiuka marufuku hiyo ikiwemo wachezaji na mameneja watapigwa faini ya shilingi milioni 1.02 fedha za kenya .
Amesema kuwa yeye mwenyewe licha ya kuwa na umri wa miaka 80 hunyoa ndevu zake.
Anasema kwa kuwa mchezaji ni sharti mtu awe mfano mwema kwa vijana.Cavcav alinukuliwa akiliambia gazeti la Uingereza la the Gurdian.
Akiongezea kuwa ndevu hizo huwafanya wachezaji hao wa soka kuwa kama wanafunzi.
Inadiwa kuwa bwana Cavcav amejaribu kulishawishi shirikisho la soka nchini Uturuki kupitia Yildirim Demiroren,ya kupiga marufuku ufugaji wa ndevu nchini humo.
''Demiroren alinimbia kwamba hawawezi kuweka marufuku hiyo kwa kuwa UEFA haitakubali.
Natamani tungekuwa na mahala pengine kwa kucheza soka alisema.
via>>BBC
via>>BBC