Baada ya kubamizwa bao 3 bila majibu,katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom na Timu ya Yanga katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga wiki iliyopita,Leo Chama la Wana,wazee wa Kalandinga wametoka sare na Wajela Jela timu ya Jeshi la Magereza nchini Prisons FC kutoka jijini Mbeya kwa bao 1-1 katika mchezo uliofanyika katika uwanja huo wa Kambarage. Prisons wamejipatia bao la kwanza katika dakika ya 7 kipindi cha pili huku Stand United wakisawazisha katika dakika ya 46 kipindi cha pili. |
Social Plugin