Kijana mmoja aliyetambuliwa kwa jina la ABDUL KOROMA Raia wa
Siera Leone Ambaye alikuwa mahabusu katika gereza la keko jijini Dar es
salaam ameuawa kwa kupigwa risasi na askari magereza katika mahakama
ya hakimu mkazi kisutu alikpokuwa akijaribu kutoroka.
Mahabusu huyo alikuwa anakabiliwa na tuhuma za Dawa za kulevya
ambapo tukio hilo limetokea baada ya mahabusu kufunguliwa kutoka kwenye
chumba cha mahabusu ya mahakama hiyo kuelekea kwenye gari la mahabusu
ambapo Mara baada ya kutoka nje alianza kutimua mbio.
Kwa mujibu wa mashuhuda walio shuhudia tukio hilo wamedai kuwa
wakati anaanza kukimbia askari magereza alifyatua risasi moja hewani
bila mafanikio ndipo akampiga ya mkononi lakini bado akawa anakimbia na
hivyo kutuka kwenye uzio kwa lengo la kukimbia Ng'ambo ya pili.
Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Suleimani Kova
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba jeshi hilo
linaendelea na uchunguzi kubaini chanzo chake
Mtu huyo alifikishwa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu kwa mara ya kwanza mwaka 2013 kwa tuhuma za kukutwa na dawa
za kulevya na kushitakiwa.
Ameuawa katika uzio wa Mahakama hiyo
baada ya kumtoroka askari magereza aliyekuwa amemsindikiza kujisaidia
ambapo alijaribu kuruka ukuta wa mahakama hiyo.
Shuhuda mmoja wa tukio hilo amesema; “alikimbilia
kwenye ule ukuta pale, akapandisha mpaka pale juu… anataka arukie
upande wa pili magereza washatokea, wakaona hawawezi kukimbia yuko mbali
ndio wakampiga zile risasi kama tatu hivi ndio akafariki…”
Akizungumzia tukio hilo Msimamizi wa Mashtaka Mahakama ya Kisutu Tumaini Kweka amesema; “Wakati wapo kwenye sero ndipo yeye akajaribu kutoroka kwa kujaribu kuruka ule ukuta wetu wa Mahakama ndipo wanausalama wetu ambao wako hapa wakaweza kundhibiti…“
Muonekano wa mahabusu aliyekuwa anatuhumiwa kubeba madawa ya kulevya, Abdul Koroma raia wa Sierra Leone baada ya kupigwa risasi.