Sheikh
Shariff Matongo akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake
jijini Dar es Salaam(hawapo pichani)kuhusu ndoto yake ambayo ameoteshwa
kuelekea mwaka 2015.
Sheikh
Sharif Matongo amesema ameoteshwa ndoto ya mwaka 2015 na kupata ushauri
kwa mashekh mbalimbali duniani ambavyo vitatokea nchini na viongozi
wasipuuze ndoto hiyo.
Sharif aliyasema hayo leo ofisini kwake
alipokutana na waandishi wa habari ,alisema ameoteshwa mambo saba
likiwemo la kupata Rais ajaye ambaye kiongozi ambaye muda mwingi ameishi
nje ya nchi kwa kufanya kazi.
Alisema
katika ndoto nyingine kitatokea kifo cha kiongozi mkubwa ambaye ameshika
nyadhifa mbalimbali na mwenye kambi katika Chama cha Mapinduzi
(CCM).
Sheikh alisema ndoto nyingine kutokea kwa mvua nyingi ambapo
watu wanaoishi mabondeni ,kutokea kwa vifo vya watoto vingi
,wafanyabiashara kupata mafanikio makubwa kwa mwaka utakaoanza kesho.
Vijana
wengi watashinda katika uchaguzi ujao na wazee wataangushwa sana ihivyo
wanatakiwa kujitokeza,katiba inayopendekezwa itapita lakini kutakuwa
na vurugu ambazo zitaibuliwa na vijana.
‘’Ndoto
yangu niliopoteshwa sikukaa nayo peke yangu niliweza kupata ushauri
kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo Mufti wa wa Abuu Dhabi,Mufti wa
Nigeria na wengine wote wanakaniambia suala hilo nisikaaye nalo
nishirikishe na watanzania wenzangu’’alisema Sheikh Shariff Matongo.
Sheikh
Shariff alisema katika usafiri wa bahari utakuwa mbaya kutokana na
bahari kuchafuka na chombo kimoja kitazama kutokana na kuchafuka huko.
Alisema
ndoto hizo ni lazima kuweza kuzingatia kutokana na kupata ushauri wa
watu wengi wenye kuaminika katika jamii katika mataifa mbalimbali
ulimwenguni.
via>> multimediawe blog
via>> multimediawe blog
Social Plugin