MSICHANA mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Jenipher,
anayedaiwa kujiuza katika maeneo ya Shivaz na Kaloleni jijini Dar es salaam,
amekutwa akiwa amepoteza fahamu kando ya barabara, katika harakati za
kujipatia chochote kipindi hiki cha sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.
Akiwa pembeni ya barabara, Jenipher anayeelezwa kuwa maarufu mjini
hapa, anadaiwa kuwa siku hiyo alizidisha idadi ya wanaume aliotoka nao,
kwa ajili ya kujipatia kipato cha kutosha ili aweze kuburudika vizuri
wakati wa sikukuu ya Krismasi.
Baadhi ya mashuhuda wanaomfahamu msichana
huyo walisema kwamba katika kipindi cha wiki nzima iliyopita, alikuwa
akisaka wanaume kwa bidii na kwamba alikuwa tayari kwa ajili ya kutoa
huduma hiyo mahali popote.
“Unajua hapa kila mtu na mambo yake, huyu Jenipher siku zote tupo
naye ila wao huwa hawaendi kulipia gesti, ila wanafanya ngono popote
hata mtaroni, kwenye ukuta ilimradi huyo mwanaume yupo tayari, ila usiku
alizidiwa na wanaume na hakuwa amekula,’’ alisema mmoja wa dada poa
aliyekataa kutaja jina lake.
Mmoja wa wamiliki wa baa iliyo maeneo hayo, aliyeomba hifadhi ya jina
lake, alisema wasichana wengi wanaojihusisha na biashara hiyo wamekuwa
na tamaa kiasi cha kushindwa kujali afya zao, kwani baadhi yao huacha
hata kula chakula, badala yake, hunywa pombe aina ya viroba.
Hadi tunatoweka eneo hilo, bado binti huyo alikuwa yupo eneo hilo akiwa hajitambui.
Social Plugin