Mwanamke mmoja nchini Marekani ameamua kumuua mwanae wa kiume wa
miaka 10 akiamini ataenda mbinguni na kukwepa matatizo ya dunia.
Mwanamke huyo mkazi wa mji wa Kansas Lindsey Blansett
mwenye miaka 33 alifunguliwa mashtaka ya mauaji baada ya kutenda kosa
hilo kwa mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Caleb wakati wakiwa
nyumbani na dada yake.
Lindsey Blansett na mwanaye Caleb enzi za uhai wake |
Polisi walisema mama huyo alimkata mtoto wake kwa kutumia kisu bila
kujali maumivu aliyoyapata na baada ya kutenda kosa hilo aliwapigia
polisi simu ili waweze kumshtaki.
Alisema alikua tayari kutumikia adhabu yoyote ile ilimradi ametimiza
lengo lake la kumuua mwanaye na kuamini ataenda Mbinguni na kukwepa
matatizo ya kidunia ambayo angekutana nayo siku za baadaye.
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba +255 688 405 951
Social Plugin