Mfanyabiashara wa nafaka mjini Katoro wilayani Geita Mkoani Geita Tatu Leonard (40) pamoja na Bibi yake Kabula Masunga (80) wameuawa kikatili kwa kucharangwa mapanga na watu wasiofahamika huku Anastazia Manogoleku (60) ambaye ni Mama yake mzazi akilazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita kwa aajili ya matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa vibaya na watu hao.
Kwamujibu wa Diwani wa kata ya Katoro Gervas Daud Kabulu alisema kuwa tukio hilo la kinyama limetokea katika kitongoji cha Ludete mjini Katoro majira ya saa mbili usiku wa kuamkia esemba 19 mwaka huu wakati wanafamilia hao wakipata chakula cha usiku .
Kabulu alisema kuwa watu zaidi ya wawili wasiofahamika wakiwa wamevalia nguo nyeusi usoni kwa lengo lakuficha sura zao walifika katika familia hiyo na kisha kuanza kuwashambulia kwa mapanga bila huruma na kisha kutokomea kusikojulikana.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Geita Dkt Adamu
Sijaona amewataja waliofariki dunia kuwa ni Tatu Leonard(40) Kabula Masunga(80) na kwambaTatu alifikishwa hospitalini akiwa amefariki na Kabula alifariki juzi asubuhi.
Dkt Sijaona watu hao walikuwa wamekatwa mapanga sehemu za kichwani na shingoni hali iyosababisha vifo vyao.
Amesema katika tukio hilo Anastazia Manogoleku(60) amejeruhiwa kichwani na kidole gumba cha mkono wa kushoto na hali yake inaendelea na matibabu katika hospitali ya wilaya ya Geita.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi unafanyika ili kufahamu chanzo cha mauaji hayo na kuwakamata wale wote waliohusika na tukio hilo na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Na Valence Robert-Malunde1 blog