Ndugu wa watu waliokuwa kwenye ndege iliyopotea wakifarijiana huku wengine wakilia kwa uchungu.
Kikosi
cha wanamaji nchini Indonesia kikisali kabla ya kuanza zoezi la
kuitafuta Ndege ya AirAsia QZ8501 katika bandari ya Pangkal Pinang
kwenye kisiwa cha Sumatra.
Kufuatia
kupotea kwa ndege ya shirika la ndege la Asia ndege namba QZ8501At
,miili arobaini imeopolewa kutoka baharini katika utafutaji wa mabaki ya
ndege hiyo na utafutaji unaendelea.
Miili hiyo iliyoonekana
ikielea karibu na taka za bahari pwani ya Indonesia,eneo la Borneo
moja ya eneo la utafutaji mabaki ya ndege hiyo.Na taarifa kutoka
serikali ya Indonesia zimethibitisha kwamba miili hiyo inatoka katika
ndege iliyopotea.
Ndege hiyo aina ya Airbus A320-200,ilikuwa
imebeba abiria mia moja na sitini na wawili ikitokea Surabaya nchini
Indonesia kuelekea Singapore,ilipotea siku ya Jumapili.
Utafutaji
wa mabaki ya ndege hiyo umeingia katika siku ya tatu,na eneo la
utafutaji limeongezwa na kufikia kanda kumi na tatu hii inashirikisha
nchi kavu na baharini.
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari
uliooneshwa wazi kwenye runinga ya taifa la Indonesia picha za taka
bahari zilioneshwa zikiwa zimechanganyika na mabaki ya miili ya abiria
ikielea majini.
Ndugu wa mabaki hayo walipoona picha hizo
walipigwa na fadhaa kuu na walionekana kushtushwa na picha hizo.Baadaye
askari wa majini nchini Indonesia wameeleza kuwa miili hiyo arobaini
iliopolewa na meli ya kivita .
Mkurugenzi mtendaji wa AirAsia
Fernandes ali ingia katika mtandao wa twitter na kueleza huzuni yake kwa
ndugu waliopoteza ndugu zao katika ndege QZ 8501. Na kwa niaba ya
shirika la ndege la AirAsia ametuma salamu za rambi rambi .
Utafutaji miili na mabaki ya ndege hiyo unashirikisha meli thelathini,ndege kumi na tano na chopa saba.
via>>BBC