Amri imetolewa ya kuwataka abiria kuondolewa kwa ferry iliyo na karibu
abiria 460 ambayo ilishika moto ilipokuwa safarini kutoka nchini Ugiriki
kwenda Italia.
Abiria waliokuwa kwneye ferry hiyo walipiga simu
kwa vituo vya runinga nchini Ugiriki wakisema kuwa mawimbi makali na
upepo unatatiza shughuli za uokoaji.
Maafisa wa ulinzi wa pwani
nchini Ugiriki wamesema kuwa ferry hiyo ya Norman Atlantic ilikuwa
umbali wa kilomita 30 kutoka kisiwa cha Othonoi wakati walipotuma ujumbe.
Vyombo vya habari nchini Italia vinasema kuwa moto ulianzia kwenye eneo la kuegesha magari.
Social Plugin