JESHI LA POLISI KAHAMA LIMEJIPANGA VYEMA MSIMU HUU WA SIKUKUU



Jeshi la polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga limetoa wito kwa wananchi wilayani humo kutoa ushirikiano na jeshi hilo kwa kutoa taarifa za uharifu ili kuimarisha ulinzi na usalama kuelekea katika sikukuu za Krismasi na mwaka mpya.

Akizungumza na   Malunde 1 blog mkuu wa kituo cha polisi wilayani Kahama Elis Ulomi amesema wananchi wana wajibu wa kushirikiana na jeshi la polisi katika kulinda amani na utulivu katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za Krismas na mwaka mpya 2015 kwa kutoa taarifa ya vyanzo vyote vya uharifu  kama wizi na uporaji wa mali zao.

Ulomi amesema  jeshi la polisi limeweka mipango madhubuti ya kuimarisha ulinzi na usalama hasa katika maeneo yote ya kumbi za starehe kama baa,na klabu, ambapo kutakuwa na walinzi wakutosha kuanzia siku ya mkesha wa Krismasi na kuendela hadi sikukuu ya mwaka mpya.

Ameongeza kuwa katika kipindi hiki cha sikukuu kumekuwepo na matukio mbalimbali kama ajari za barabarani pamoja na baadhi ya wananchi katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo kuvamiwa na kuporwa mali zao na hivyo kuwaomba wananchi wote kuwa waangalifu  katika kipindi hiki ili waweze kusheherekea sikukuu hizo kwa amani na utulivu.

“Jeshi la polisi tumejipanga vizuri na niwatoe hofu wananchi wote  wilayani Kahama washeherekee kwa amani na uhuru  siku ya sikukuu kwani ulinzi utakuwepo wa kutosha katika maeneo yote,nawatakia sikukuu njema na mungu awabariki”alisema Ulomu.

Sikukuu ya Krisimas huadhimishwa Disemba25 kila mwaka ambayo ni sikukuu ya kiimani kwa wakristo wote duniani kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mwokozi Yesu kristo,hali kadhalika sikukuu ya mwaka mpya huadhimishwa Januari mosi kila mwaka ikiwa ni mwanzo wa mwaka mpya .

Na Philipo chimi-Malunde1 blog Kahama

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post